'Kuliko' na 'Kushinda'

Matumizi ya kuliko na kushinda

Kuliko na kushinda hutumika kuonyeshea kuwa, jambo/kitu/hali moja imezidi au imepita ile nyingine.

  • Kwa mfano, iwapo mimi nina bidii kumzidi mwenzangu Juma, basi tutasema: Mimi nina bidii kuliko Juma au Mimi nina bidii kumshinda Juma.

Kuliko linapotumika, kiwakilishi chochote cha nafsi hakiwekwi katikati ya neno kuliko. Yaani: tunasema sio kuliko mimi kuniliko kuliko sisi kutuliko kuliko nyinyi kuwaliko kuliko yeye kuwaliko.

Muhtasari wa ngeli