Matumizi ya 'huku'

Huku hutumika kwa njia tatu:

  • Huku ya mahali; Huku shuleni kunapendeza. Huku tunakosomea ni kutulivu.

  •  Huku ya wakati Huonyeshea kuwa vitendo viwili vinafanyika wakati mmoja: k.m. Nyanya alituhadithia huku akipika ugali; Huku akiongea, mwalimu aliandika ubaoni.
  •  Huku ya kiashiria Hutumika katika ngeli ya KU-KU kuashiria, vitenzi Kucheza huku kunapendeza. Kusoma huku kunafaidi.