Koma

Koma/kituo/mkato ( , )

Hutumika:

  • Mahali msomaji anapopumua au anapotua. k.m.

Nilipokula na kushiba, nilifunganya virago vyangu na kuondoka.

  • Tunapoandika anwani:

Shule ya Bidii,

S.L.P. 20400,

HOMA BAY.

  • Kutenganisha orodha ya maneno. k.m

Alinunua mkate, maziwa sukari na kahawa.

  • Kutenganisha sentensi za masharti k.m.

Nikijitahidi, nitafua dafu.