Nukta na koma

Nukta na koma ( ; )

Hutumika:

  • Kutenganisha sehemu kuu ya sentensi. k.m. Nilipozinduka, nilimsikia jirani yangu akipiga kamsa; yawezekana alikuwa katika hatari fulani.
  • Kutenga sentensi ndefu. Kadzo alimpelekea vitu vya thamani si hafifu; kama angevikosa bila shaka angenung'unika.