Kituo kikuu

Kituo kikuu/nukta/kikomo/kitone ( . )

Hutumika:

  • Mwishoni mwa sentensi: k.m tutafika alfajiri na mapema.
  • Kufupisha maneno: S.L.P. (Sanduku la posta).

Bw. Juma (Bwana Juma)

  • Kutenga kiwango cha kitu kama vile fedha, kilomita, kilo n.k. Sh 6.80 (shilingi sita na senti themanini).
  • Kilomita 2.5 (kilomita mbili na nusu).