Kiambishi - 'na' pamoja na kirejeleshi

Tazama sentensi zifuatazo:

  • Kitabu kisomwacho ni kipya.

  •  Vitabu visomwavyo ni vipya.

 Kitabu asomacho ni kipya. Ukizingatia sentensi hizi mbili, utagundua kuwa, katika sentensi ya kwanza kiambishi ni ki (kinachowakilisha kitabu).

Katika sentensi ya pili, kiambishi ni a (kinachowakilisha msomaji). Tofauti hii ya viambishi imetokana na mnyambuliko wa kiarifu (kitenzi) kilichotumika. -somwa -

Hali ya kutendwa. -soma -

Hali ya kutenda.

  • Iwapo kitenzi kimo katika hali ya kutendwa, kiambishi kitakachotumika kitawakilisha nomino husika. (Nomino inayotendwa yaani nomino ionyeshwayo katika sentensi).
  • Iwapo kiarifa au kitenzi kimo katika hali ya kutenda, kiambishi kinawakilisha mtenda (nomino ambayo kwa kawaida haionyeshwi katika sentensi).

Angalia mifano hii kwa makini.