Ngeli ya PA - PA

- Ngeli ya PA huonyesha mahali HAPA, HAPO, PALE, ambapo ni mahali dhahiri, au wazi panapoeleweka au ambapo tuna habari kupahusu hata kama penyewe ni mbali. 

- Viarifu vya ngeli hii huanza kwa pa- k.m Darasani panapambwa kwa matayarisho. 

N/B Jina lolote linaweza kupachikwa kiambishi tamati -ni, nalo likawa au likageuka kuwa mahali HAPA, HAPO, PALE. 

Mifano: 

a) Nyumbani hapa pana vyakula vingi.

b) Nyumbani hapo pana vyakula vingi.

c) Nyumbani pale pana vyakula vingi.

Vivumishi

Viwakilishi amba-

Sakafuni ambapo anafagia panateleza.

1. 'O' rejeshi

Sakafuni anapofagia panateleza.

2. 'Ndi' ya kusisitiza

Hamamuni anapooga ndipo hapa.

3. 'Si-' ya kukataa

Hamamuni anapo ogea sipo hapa.

4. 'Na-' ya kirejelei

Hapa napo pana watoto wengi.

 

5. Viashiria/vionyeshi: hapa, hapo, pale.

  • Viashiria/vionyeshi radidi

hapa hapa, hapo hapo, pale pale.

  • Viashiria/vionyeshi visisitizi

papa hapa, papo hapo, pale pale.

 

6. Kivumishi -enye

Sokoni penye wateja pana kelele. 


7. Kivumishi -enyewe

Tuliogelea mtoni penyewe


8. Kivumishi -ote

Mezani pote pana vitabu.

9. Kivumishi -o-ote

Nitakaa popote nitakapoonyeshwa.


10. Kivumishi -ngi 

Hotelini pengi pana starehe. 


11. Kivumishi -ngine 

Alienda hotelini pengine palipompendeza 

12. Kiulizi -pi? 

Mjomba alienda shuleni papi

Matumizi ya viambishi vya PA katika sentensi 

1. Kiambishingeli (pa) 

Nyumbani pale pananipengeza - Nyumbani pale panatupendeza.

 

2. Kirejeshi -O (-po)

Shuleni palipofyekwa ni pangu. - Shuleni palopofyekwa ni petu.

 

3. Kiunganifu -A (pa)

Kitandani pa mtoto panafaa. - Vitandani pa watoto panafaa. 

 

4. Sifa -enye/-enyewe

Chumbani penyewe pana baridi. - Vyumbani penyewe pana baridi.

Ubongoni penye nia pana njia. - Ubongoni penye nia pana njia.

 

5. Sifa (-ote, -o-ote)

Dukani pote pana bidhaa. - Madukani pote pana bidhaa.

Uwanjani popote mtu hununua bidhaa. - Nyanjani popote panafaa.

 

6. Sifa (-eupe, -eusi, -embamba)

Tunduni pembamba pana mende mdogo. - Matunduni pembamba pana mende wadogo.

 

 7. Sifa -ngi, -ngine

Ukutani pengine pana rangi. - Kutani pengine pana rangi.

Ukutani kwingi kuna rangi. - Kutani kwingi kuna rangi.

 

8. Vivumishi -pa

Jikoni pazuri pakubwa pana mlo. - Majikoni pazuri pakubwa pana mlo. 

 

9. Kukanusha hapa-,

Uwanjani hapo hapana unyasi mrefu. - Nyanjani hapo hapana nyasi ndefu. 

 

ZOEZI 

Tia sentensi zifuatazo katika ngeli ya mahali (PA) kulingana na kiambishingeli ulichopewa mabanoni. 

Mfano: Nyumba yangu ni nzuri = Nyumbani pangu ni pazuri. 

1. Mlango ule una bawabu mkali. 

2. Mlima wote umetanda ukungu. 

3. Mto ule mkubwa una ngwena wakubwa. 

4. Katika kisima kile mna maji safi. 

5. Dika nilipendalo lina bidhaa marighawa. 

6. Msitu wote ule waliuoalilia jana. 

7. Anayelilima shamba hili hajalimaliza. 

8. Gari lile jeupe limeibeba mizigo mingi. 

9. Kitanda chako kizuri ndicho nitakachokilalia. 

10. Maskani yoyote yakufaayo uyakimbilie, usisite.