Ngeli ya Mahali

Ngeli ya mahali

Ngeli ya mahali hujumuisha nomino za mahali. Nomino za mahali hupatikana kwa kuongeza silabi ni mwishoni mwa baadhi ya nomino za vitu k.m. meza ni kitu lakini tukiongeza silabi niinakuwamezani – mahali.

Mifano ya nomino za mahali ni: nyumbani, sokoni, kituoni, chuoni, mtoni, kitini, maegeshoni, darasani, msalani, jikoni, kichwani, sakafuni. n.k.

Kwa kawaida, ngeli ya mahali hugawanyika katika sehemu tatu.

  1. Ngeli ya mahali ya MU-MU
  2. Ngeli ya mahali ya PA-PA
  3.  Ngeli ya mahali ya KU-KU. Muhimu Ngeli ya KU-KU ni ya kipekee kwani ndiyo ngeli pekee inayojumuisha vitenzi tuvinavyoanza kwa silabi ku.