Ngeli ya I - I

- Ngeli hii hujumuisha nomino za vitu visivyo na uhai.

- Nomino hizo zinatumia vivumishi sawa katika hali ya umoja na wingi. Kwa kawaida vitu vya nomino katika ngeli hii haviwezi kuhesabika wala kugawika k.m. hewa, mvua, baridi, giza, chai, furaha, huzuni.

Vivumishi Vivumishi vya ngeli hii ni sawa na vivumishi vya ngeli ya I - ZI (hali ya umoja).

C. Jaza jedwali lifuatalo

 

Matumizi ya viambishi katika ngeli ya I - I

1) Viambishingeli (i - i)

i) Mihadarati inaathiri afya ya anayeitumia.   -   Mihadarati inaathiri afya za wanaoitumia.

ii) Midadi ilimwagikia daftari langu.   -   Midadi ilimwagikia madaftari yetu.

2) Kirejeshi -O (yo - yo)

i) Miwani iliyonunuliwa ndiyo yangu.   -  Miwani iliyonunuliwa ndiyo yetu.

ii) Miraa ambayo ambayo aliitafuna imemlevya. - Miraa ambayo waliitafuna imewalevya.

 

3) Kiunganifu -A (ya - ya)

i) Mizani ya shairi hili ni hii.   - Mizani ya mashairi haya ni hii.

ii) Miadi ya jana nimeitiniza.   -   Miadi ya jana tumeitimiza.

 

4) Sifa -enye na -enyewe (ye - ye)

i) Miwani yenye kioo kizuri imeanguka.   -   Miwani yenye vioo vizuri imeanguka.

ii) Mirathi yenyewe ni ya mtoto.   -   Mirathi yenyewe ni ya watoto.

 

5. Sifa -ote na o-o-te (yo - yo)

i) Minenguo yake yote inavutia.   -   Minenguo yao yote inavutia.

ii) Mirabaraba  yoyote ya nguo hii inapendeza.   -   Mirabara yoyote ya nguo hizi inapendeza.

 

6) Sifa -eusi, -eupe n.k. (mie - mie)

i) Miwani yako mieusi iko wapi?   -   Miwani yenu mieusi iko wapi?

ii) Mirimo miema ni ya kuijenga nchi.   -   Mirimo miema ni ya kujenga nchi.