Kiambishi na kirejelei cha mwisho

Kulingana na nyakati, kirejelei kinaweza kutumika katikati ya kiarifu au mwishoni mwa kiarifa. k.m.

  • Mtoto anayecheza (wakati uliopo).

  •  Mtoto aliyecheza (wakati uliopita).

  • Mtoto atakayecheza (wakati ujao).

  • Mtoto achezaye (wakati wa mazoea).

Kiambishi na kirejelei cha mwisho hutegemea mambo mawili:

  •  Ngeli ya nomino husika.
  •  Mnyambuliko wa kiarifa husika.

Tazama mifano hii

  • Mchezo achezao (kufanya)
  • Mchezo uchezwao (kufanywa) Katika mfano wa kwanza, kiambishi (a) kinawakilisha mtendaji yaani achezaye ilhali katika mfano wa pili kiambishi (u) kinawakilisha kitendewa yaani mchezo.