Maswali kadirifu

Viambishingeli

Ngeli ya A - WA na LI - YA

A. Maneno yafuatayo yanapatikana katika ngeli gani? 

  1. mtu
  2. kipepeo
  3. babu
  4. tarishi
  5. neno
  6. kasisi
  7. jiwe
  8. jembe
  9. jiko
  10. balozi

 

B. Tumia viambishngeli mwafaka kujaza mapengo katika sentensi zifuatazo.

1. Mbuzi ___ nayecheau ni wangu.

2. Kiamboni ___ namoimbwa ni mwetu.

3. Tunda ___ naanguka.

4. Mkate ___ tanunuliwa.

5. Maiti ___ tazikwa kesho.

6. Kusoma ___ naendelea.

7. Ukuta ___ tapakwa rangi.

8. Urefu wake ___ namsaidia mchezoni.

9. Sokoni mote ___ na takataka.

10. Kikosi cha askari ___ mefika.

 

C. Tumia viambishi mwafaka kujaliza mapengo katika sentensi zifuatazo

1. Majina yote ___ tasomwa.

2. Nyanya ___ nauzwa.

3. Mizozano ___ mekoma.

4. Ng'ombe hao ___ tauzwa.

5. Vifungu vya matunda ___ metengwa.

6. Ulevi ___ nahatarisha maisha.

7. Vyeti ___ tatili sahihi.

8. Karatasi yote ___ tapigwa cxhapa

9. Wifi ___ nakula.

10. Daktari ___ tamtibu.

 

Ngeli ya U - I na YA - YA

A. Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo.

1. mkono      2. marashi

3. mti           4. mgomba

5. manukati   6. mate

7. mafuta      8. mchungwa

9. maji         10. mhindi

 

NOMINO

A. Taja aina sita za nomino.

1.

2.

3.

4.

5.

6.

 

B. Tambua nomino katika sentensi zifuatazo:

1. Mwana umleavyo ndivyo akuavyo.

2. Mwalimu Tatu ni stadi wa sarufi.

3. Kata pua uunge wajihi.

4. Sijui lini kwani hakunitajia tarehe ya marejeo

5. Kitabu hiki changu chapendeza zaidi.

 

C. Kamilishi jedwali hili kwa kutaja nomino mguso na nomino dhahania

Nomino mguso ni zile za kushikika au kugusika na nomino dhahania ni zile ambazo hazishikiki kamwe.

Nomino mguso                     Nomino dhadhania

meza kalamu                        amani upendo

1.                                              1.______

2.                                              2.______

3.                                              3.______

4.                                              4.______

5.                                              5.______

 

D. Nomino za kiasi

Kamilisha nomino za aria au kiasi (makundi)

  1. ubale wa _____
  2. silesi ya _____
  3. kigae cha _____
  4. chinyango ya _____
  5. kigunzi cha _____
  6. tembe ya _____
  7. donge la _____
  8. kiraka cha _____
  9. mnofu wa _____
  10. ufefe wa _____

 

E. Chagua jibu sahihi kujaliza kila pengo

1. Rangi ya mbingu huwa _____ (samawati, kijivu).

2. Mwanaume mzee sana huitwa _____ ( rijali, buda).

3. Tita la kuni,kivunga cha _____ ( maji, nywele).

4. Kamilisha sentensi kwa kivumishi sahihi.

5. Embe hili ni _____ ( jororo, jeroro).

6. Gari lilochakaa huitwa _____ ( kitangabari, katara).

7. Mkono wa kushoto ni wa _____ ( yamini, shemali).

8. Shairi la mshororo mmoja huitwa _____ ( tathnia,tathmina).

9. Lo!Salaala!,aka !,shabash! Maneno ya aina hii huitwa _____ (viingizi,viigizi )

10. Shuleni, polepole,adhuhuri,kistadi:Haya ni aina gani ya maneno? ( viarifa, vielezi )

11. Moto hurindima, ndege _____ ( hukorokocha,hutatalika).

12. Barua rasmi ina anwani _____  ( thelatha,thenine).

13.Robota la pamba,matopa ya _____ (nyanya,vitabu).

14. Moto hurindima,ndege _____ (hukorokocha, hutatalika).

15. Je,maana ya nahau,'anayelaza damu' ni nini? _____ (mzembe,mroho)

 

F. Badilisha vitenzi vilivyopigwa mistari viwe katika kauli ya kutendeka.

1. Nguo ilichafuliwa.

2. Wimbo uliimbwa vyema.

3. Ngazi ilitengenezwa tena

4. Sakafu ilikarabatiwa upya.

5. Maji yalizolewa yalipomwagwa.

Vivumishi sugu / visivyochukua viambishi

Hivi vivumishi visivyochukua viambishi vya ngeli:kwa mfano,gani ,safi, nadhifu, hodari na vinginevyo.

A. Andika sentensi zifuatazo katika wingi.

1. Mtu gani amefika?

2. Yeye ni hodari.

3. Anakutumia kitambaa safi.

4. Mgonjwa dhaifu amepewa dawa.

5. Gari hilo ni ghali mno

6. Aliniuliza maswali rahisi

7. Mjomba wangu ni bingwa wa kuogelea

8. Koti lake ni laini.

9. Wazo lake lilikuwa duni.

10.Yeye ni mtu mahiri.

 

B. Teau jibu sahihi ili kujaza kila pengo.

  1. Tulipika vyakula _____. (vibora,bora )
  2. Wale ni watu _____ . (sita, wasita )
  3. Walimwuliza maswali _____ ( gani, magani)?
  4. Alikuwa na matunda _____ ( haba, mahaba).
  5. Yule ni mtu _____ (mtajiri , tajiri)
  6. Tulitumia vitabu _____  (tele, vitele)
  7. Mishipi kumi na _____ imenunuliwa ( misababa, saba).
  8. Hiyo ni miti _____ (mihafifu, hafifu)
  9. Ana mawazo _____ (maduni, duni)
  10. Hao ni watu _____ (katili, wakatili).

 

Kirejeshi amba -

A. Jaza kila pengo kwa kutumia 'amba-' kwa usahihi.

Ng'ombe _____ anakimbia ni mnono.

Kisu _____ kilitumika ni butu.

Jani _____ limeanguka limekauka.

Uteo _____ anautumia si mpya.

Mwongo _____ ulipita ulionekana mrefu

Uzalendo _____ alionyesha ulivutia wengi.

Kengele _____ anatumia ni mbovu.

Ubele _____ umeng'oka ni wa kuku.

Furaha _____ alionyesha ilizidi.

Darajani _____ ajali ilitokea pamekarabatiwa.

 

B. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya umoja

1. Meno ambayo yaliuma yalitiwa dawa.

2. Kalamu ambazo tulizitumia zilipendeza.

3. Nyoka ambao wan sumu ni hatari.

4. Vyombo ambavyo vilinunuliwa vilirudishwa.

5. Nyaraka ambazo waliziandika zolifurahisha

 

C. Taja jinsi 'ni' imetumika katika sentensi zifuatazo

  1. Mimi ni mwalimu.
  2. Someni kwa bidii!
  3. Mjomba ameenda mtoni.
  4. Ninajitahidi nifanikiwe
  5. Nilikoroma nikiwa usingizini.
  6. Jirani yangu ni mpole.
  7. Njooni hapa!
  8. Imbeni kwa furaha!
  9. Alinipa zawadi baada ya ushindi wangu.
  10. Alienda mjini kutafuta kazi.

Matumizi ya 'katika' na 'kwenye'

A Tumia 'katika' au 'kwenye' kujaza pengo

1. Bidii _____ elimu humwezesha mwanafunzi kufanikiwa.

2. Kuiga ____ maafa ni  huko.

3. Alisimama _____ barabara kusubiri gari.

4. Joka aliingia  _____ shimo.

5. _____ fijo hakupendezi.

 

B. Zisahihishe sentensi zifuatazo.

  1. Tulisafiri hadi katika sokoni
  2. Alingia ndani mwa bafuni
  3. Mambo mengi yanapatikana kwenye kitabu hiki.
  4. Aliingia ndani ya nyumbani.
  5. Tulikuwa katika uwanjani.

Matumizi ya kiunganishi 'na'

  • Wana vitabu vizuri
  • Mimi nina furaha na amani.
  • Musa alinunua mkate na soda
  • Tunaishi na shangazi yetu.
  • Watoto walishikana wakaangushana.

      6. Ni kiunganishi kipi huonyesha hali ya hitilafu

         A. Pindi

         B. Kati ya

         C. Maadamu

         D. Lakini

Vielezi

Vielezi vya mkazo

A.Teau vielezi vya mkazo kujazia mapengo yanayofuata

1. Yeye ni maskini _____ . Hana bee wala tee.

2. Tuliingiwa na _____ tulipopokea habari za kupona kwake.

3. _____ tulikaa pale tukimsubiri mwizi ajitokeze . Hata hivyo hakujitokeza.

4. Waalikwa hao walizusha _____ huko karamuni walipolewa chakari.

5. Bidii zao zote zilikuwa _____ kwani hawakupata walichotarajia.

6. Maskini mtoto huyo alipoingia,alipeleka _____ lakini bado hakupata nafuu.

7. Mwalimu wetu alitueleza _____ kuhusu maafa ya ukimwi.

8. Wao ni marafiki wa _____.

9. Safari yetu ya _____ ilituchosha sana.

10. Mtoto huyo alilelewa kwa ____ hadi alipokuwa mtu mzima.

11. _____ zilihanikiza kote hewani bao la ushindi lilipofungwa.

12. Tangu _____ jamii hiyo imeshi katika eneo hilo.

13. Kijana huyo _____ .Uzembe wake umepita mipaka.

14. Tulitafuta pesa za kununulia vitabu kwa _____.

15. Tulikumbana na _____ mafuriko yalipokumba kijiji chetu.

16. Maskini mjomba aliingiwa na _____ aliposikia mtoto wake ametiwa mbaroni kwa hata ya wizi.

17. Tangu apigwe kalamu, hana _____.

18. _____ alipomwona mwanawe akivuta sigara chooni.

19. Mzee huyo aliadhibiwa _____ .Kumbe hii dunia ya mnyonge msonge!

20. Licha ya kukanywa kutoenda shereheni hakukanyika. Alisema angeenda na _____.

Viulizi

A. Tumia  kiulizi "ngapi" kwa usahihi kujaza pengo.

  1. Amekata kiti _____?
  2. Ni vifranga _____ huanguliwa kila siku?
  3. Myoto _____ imezimwa?
  4. Ni mafundi ____ hufanya kazi hii?
  5. Je, wote walikuwa _____?

 

B. Tumia kiulizi "-pi" kwa usahihi kujaza pengo.

  • Jopo ____ lilikiandika kitabu hiki?
  • Tutainunua keki ____ ya sherehe?
  • Ni aina _____ za vyakula unapendelea?
  • Ni walemavu waliopata msaada?
  • Ubao _____ ulipakwa rangi?

Vihisishi

Lo!            Aka!

Taib!          Ebo!

Po!            Astafullah!

Haya!        WallahI!

Habedari!   Kefle!

 

Viunganishi

A. Teau viunganishi mwafaka kujibia maswali yafuatayo

ndiposa, kwa ajili, hadi, baada ya, ndiposa

  1. Mtoto alilia _____ aonewe huruma
  2. _____ maombi tulingo'a nanga
  3. Wageni watakaa kwetu ____ kesho jioni
  4. Walifika _____ ya kumliwaza.
  5. Alienda kucheza huko barabarani ____ alikuwa amekanywa.

Nomino

ukubwa na udogo wa nomino

A. Andika sentensi hizi katika ukubwa.

  • Mtoto huyu anasoma.
  • Ng'ombe wangu anakamwa
  • Kikombe kimeletwa.
  • Chumba chenyewe kinapendeza
  • Mkono wake umepona

 

Kuakifisha

Tumia alama zifuatazo kwa usahihi katika sentensi

  • kiulizi
  • koma na nukta
  • kistari kifupi
  • mabano
  • kihisi
  • mkwaju
  • ritifaa
  • kiyuo
  • herufi kubwa
  • alama ya dukuduku

Ngeli ya Ku - Ku na Pa - Ku - Mu

Ngeli ya Ku-ku hutokana na vitenzi - jina.

Ngeli ya Pa-Ku-Mu ni ya mahali

Onyesha viambishingeli katika sentensi zifuatazo.

  1. Kucheza kwake ni kuzuri
  2. Kuandika kubaya hakupendezi.
  3. Kuzungumza vizuri kunavutia.
  4. Pahali pake ni pema.
  5. Mahali mwake mnavutia.
  6. Alimoingia mnapendeza.
  7. Aliko hakukaliki.
  8. Kwenyewe ni kuzuri
  9. Mahali palipakwa rangi vizuri.
  10. Kuangalia kwake kunatisha.

Usemi halisi na usemi wa taarifa

A. Ziandike sentensi zifuatazo katika usemi wa taarifa.

1. " Leo nitaelekea mjini," Musa alisema.

2. " Nguo yangu haijakauka," dada yangu alisema.

3. "Ukijitahidi utafua dafu maishani",mwalimu alimshauri mwanafunzi.

4. "Kwa nini hujamaliza chakula chako?" Mama alimwuliza mtoto.

5. "Sisi tunastahili kuondoka kesho kuelekea Mombasa,"watalii walisema

6. " Lo! Kumbe yeye ni gwiji wa Kiswahili!" Wageni walishangaa

7. "Tunashirikiana na wenzetu ili tufikie malengo yetu,"wanakijiji walisema.

8. "Kitabu hiki ni cha jirani yangu," Kazungu alisema.

9. " Visa vya ajira za watoto vimezidi katika  kata hii. Msikubali hali hii iendelee," chifu alisema.

10."Sasa unafuatana na watoto wazuri," mzazi wangu alinieleza.

MASWALI

A. Andika kinyume:-

1.Kinyume

Kitwana aliyepewa kazi ya ufalme alifurahi.

A. Kijakazi aliyepewa kazi ya umalkia alikasirika.

B. Kijakazi aliyepewa kazi ya ufalme alifurahi

C. Kijakazi aliyenyimwa kazi ya umalkia aliudhika

D. Kijakazi aliyenyimwa kazi ya malkia aligurahi

 

2. Changua jibu lililo na katika ya hali.

A. Wawindaji wamejificha  katika pango

B. Katika kuimba kwake alivutia wengi.

C. Ameongea katika muda wa saa nzima.

D. Katika mwaka mvua  huo ilipungua.

 

3.Chagua sentensi yenye kiwakilishi.

A. Wao wanalima

B. Miche mingapi imepandwa?

C. Mbona hawaongei?

D. Je, umewaona wahandisi wowote?

 

4.Andika katiaka wingi :-

Ua hilo lilimea karibu na ua ule mrefu.

A. Maua yale yalimea karibu na maua yale marefu.

B. Maua yale yalimea karibu na nyua zile ndefu.

C. Maua yale yalimea karibu na nyua hizo mirefu.

D. Nyua hizo ndefu zilimea karibu na maua yale marefu.

 

5. Onyesha kielezi

Ndege mdogo amepaaa angani.

A. mdogo    B. amepaa

C. Ndege     D. angani

 

6. Kipi ni kiunganishi cha utenzi?

A. Pengine     B. Ama

C. Mbali na     D. Ikiwa

 

7. Neno masizi liko katika ngeli gani?

A.Ya-YA     B. LI-YA

C. I-ZI         D. U-ZI

 

8. Iandike sentensi ifuatayo katika wingi hali ya wastani.

Guu lake ni kubwa

A. Mguu lake ni mkubwa.

B. Viguu vyao ni vikubwa.

C. Miguu yao ni mikubwa.

D. Maguu yao ni makubwa.

 

Kuanzia swali la 9 mpaka 24 , chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo.

9. Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa "Umekula leo?"Mama aliuliza.

A. Mama aliuliza kama amekula leo.

B. Mma alitaka kujua kama alikuwa amekula siku hiyo.

C. Mama alitaka kujua kama amekula leo.

D. Mama alitaka kujua kama angekula siku hiyo.

 

10. Kanusha sentensi ifuatayo:

Kuimba kwake kumetufurahisha.

A. Kuimba kwakw hakukuitufahisha.

B. Kuimba kwake hatukufurahia.

C. Kutoimba kwake hakujatufurahisha

D. Kutoimba kwa hakukutufurahisha.

 

11. Ni sentensi ipi sahihi kati ya hizi?

A. Ningalikusomesha ungepita

B. Ningelikusomesha ungelipita.

C. Ningalikusomesha ungalipita

D. Ningekusomesha ungalipita.

 

12. Kati ya sentensi hizi ipi inayoonyesha -po- ya mahali?

A. Kamau alipoketi alianza kusoma

B. Alipewa zawadi alipopasi mtihani.

C. Alipoketi mtoto pataoshwa asubuhi.

D. Mama aliponunua matunda alifungwa

 

13. Badilisha sentensi hii katika ukubwa wingi:

Kijiko kilichonunuliwa na mke wake kimevunjika.

A. Majiko yaliyonunuliwa na majike yake yamevunjika.

B. Majijiko yaliyonunuliwa na majike yao yamevunjika.

C. Majijiko yaliyonunuliwa na jike lao yamevunjika

D. Majiko yaliyonunuliwa na majike yao yamevunjika.

 

14. Ni sentensi ipi iliyo na "KWA" ya kumiliki?

A. Wake na waume wa kijiji chetu wanakutana.

B. Juma atarithi sabini kwa mia ya mali ya kakake.

C. Mtaishi na kula kwa shangazi yenu tangu leo.

D. Kwao hakuendeki madhali baba yenu mi simba

 

15. Tambua aina ya maneno yaliyopigiwa mistari 

Mtoto alinunuliwa kiti kizuri sana kwa utiifu wake.

A. Kivumishi,kivumishi, kielezi

B. Kivumishi, kivumishi, nomino.

C. Kivumishi, kielezi, nomino.

D. Kielezi, kivumishi, kitenzi

 

16. Chagua muungano sahihi wa sentensi hizi.

Mgonjwa haoni. Mgonjwa hasikii.

A. Mgonjwa haoni na kusikia

B. Mgonjwa haoni maadamu hasikii.

C. Mgonjwa haoni wala hasikii.

D. Mgonjwa haoni ingawa hasikii.

 

17.Chagua sentensi inayoonyesha hali ya kutendesha.

A. Rais ametangaza vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati

B. Mchanja kuni amakaza kamba ili kuni zisidondoke.

C. Chakula hicho kilimtosha mtoto wa shangazi

D. Kumbe ni yaya amemliza mtoto wa Amina.

 

18. Badilisha sentensi hii katika udogo umoja:

Ndege wazuri walitua mitini.

A. Kidege kizuri kilitua kijitini.

B. Kidege mzuri kilitua kijitini

C. Videge vizuri vilitua vijitini

D. Videge wazuri walitua kitini

 

19. Chagua sentensi yenye kielezi ch jinsi

A. Maskauti walitembea kwa uchovu hadi kiambini.

B. Mwalimu ametoa maelezo mara ishirini.

C. Mayowe mendi yametokea gwarideni.

D. Mtihani utafanywa mwakani.

 

20. Ni sentensi gani imekanushwa katika hali tegemezi?

A. Mvua isiponyesha kwa wakati mimea itanyauka.

B. Wageni hawajafika hotelini walikotarajiwa.

C. Mjomba anapokuja hatuletei zawadi kama zamani

D. Juma asingesoma kwa bidii asingekuwa  meneja sasa

 

21. Chagua sentensi isiyoafikiana na nyingine

A. Wanafunzi wenyewe wamefaulu mtihani.

B. Wanafunzi wengine wamefaulu mtihani.

C. Wanafunzi wanane wamefaulu mtihani.

D. Wanafunzi wote wamefaulu mtihani.

 

22. Changua neno lililoambatanishwa na wingi wake.

A. Ajira - majira

B. Tikiti - matikiti

C. Sala - msala

D. Kazi - makazi

 

23. Kivumishi kutokana na kitenzi amini ni

A. amani. B. aminifu.

C. aminika. D. aminisha.

 

24. Chagua jibu ambalo mtendaji amefanya kitendo kwa niaba ya mwingine.

A. Shaaban aliwaandikia watu vitabu bora.

B. Shamba letu lilimwa na vibarua

C. Shangazi alimpokelea mama wageni

D. Sharubati imemwagikia mgeni begani

Jibu maswali chagua jibu lililo sahihi.

25. Ni kiunganishi kipi huonyesha hali hitilafu?

A. Pindi          B. Kati ya

C. Maadamu   D. Lakini

 

26. Sentensi ipi ni sahihi?

A. Nilitaka sana kuja kukusalimia mbali sikuweza

B. Walijitahidi ila wafanikiwe

C. Tulisoma ili tuelimike

D. Walifika na hawakumwona mwenyeji