Mnyambuliko wa vitenzi

- Mnyambuliko wa vitenzi ni jinsi vitenzi vinavyobadilika kulingana na kauli/hali mbalimbali.

- Kwa mfano kutokana na kitenzi 'soma' tunawezapata somea, somewa, somwa n.k. Ni vizuri kuelewa kwamba sio vitenzi vyote vinavyonyambulika katika kila kauli.

- Kwa sasa tutaangalia kauli zifuatazo. Ili kukusaidia uelewe kauli hizi vizuri, tutakutumia wewe kama mfano na mtu mwengine; lakini mnyambuliko unaweza kutumika kwa kitu chochote kila. :

  1. Kauli ya Kutenda - kitendo katika hali yake ya kawaida (bila kunyambuliwa)
  2. Kauli ya Kutendea - kufanya kitendo kwa niaba(au kwa ajili) ya mtu mwengine
  3. Kauli ya Kutendana - unamfanya mtu kitendo, naye anakufanya vivyo hivyo
  4. Kauli ya Kutendeana - unafanya kitendo kwa niaba mtu, naye anafanya kitendo hicho kwa niaba yako.
  5. Kauli ya Kutendwa - kuathirika moja kwa moja na kitendo
  6. Kauli ya Kutendewa - kitendo kufanywa kwa niaba yako au kwa ajili yako.
  7. Kauli ya Kutendeka - kitendo kukamilika au kuwa katika hali timilifu
  8. Kauli ya Kutendesha - kumfanya mtu atende jambo fulani
  9. Kauli ya Kutendeshana - mtu anakufanya utende jambo fulani, nawe unamfanya atende jambo lilo hilo

Mifano Katika Jedwali

Zoezi

1. Harakati za kutetea haki watoto zili ____ (pita) mwaka 2001.

2. Watoto wanapaswa _____ (kula) vizuri.

3. Vitabu vyote uvi_____ mkobani uende navyo.

4. Tabia mbaya na ukosefu wa nidhamu huwa _____ ( chukia) wazazi.

5. Tunda lililooza ni muhali ____ (kula) kabisa.

6.Wazazi ____ (lazimu) kuwapeleka watoto wao shuleni.

7. Pahali penye uchafu hapafai ____ ( kaa) maishani.

8. Uhasama ____ (toa) watu wakipendana.

9. Jiko hili la umeme ndilo lililoya _____ (chemka) nikapiga chafya.

10. Mwanafunzi ame ____ (kumbuka) kuyajibu maswali kwa makini.

11. Wanakijiji wali _____ (eleza) wapande miti mingi.