Kitenzi

Kitenzi

Kitenzi ni neno ambalo hutumika kutujulisha tendo linalofanyika. Baadhi ya vitenzi ni kama vile: Lia, cheka, lala, amka, soma, kimbia n.k.

Kitenzi kinaweza kuchukua kiambishi awali ku k.m. Kulia, kucheka, kulala, kuamka, kusoma, kukimbia n.k.

Iwapo kitenzi kitachukua kiambishi awali ku basi kitenzi hicho kitawekwa katika ngeli ya KU - KU.