Usemi wa kauli halisi

- Usemi wa kauli halisi pia huitwa usemi wa moja kwa moja.

- Katika usemi huu maneno ya msemaji hunukuliwa moja kwa moja jinsi alivyoyatamka. Kwa hivyo, sheria fulani huzingatiwa.

  • Alama za kunukuu hutumika k.m. “Kitabu hiki ni changu,“ mwanafunzi alisema.

  • Alama za kuulizia hutumika k.m. “Je, umemwona Hamisi?” dada aliuliza.
  •  Alama za hisi hutumika k.m. “Lo! Hamwogopi nyoka!” Mwalimu alishangaa.

  •  Wakati wowote hutumika k.m. “Nitaenda Mombasa,” shangazi alisema; “Walifika jana,” mwenyeji alieleza. Katika matumizi ya kauli halisi wanafunzi hukumbana na tatizo moja sugu: jinsi ya kutumia herufi kubwa, koma na kikomo.

Tazama sentensi zifuatazo:

  1.  Mama alisema, “Leta kikombe.”
  2. “Leta kikombe,” mama alisema. Ukiziangalia sentensi hizi mbili, utaona kuwa, matumizi ya koma na kikomo ni tofauti.

Ukiziangalia sentensi hizi mbili, utaona kuwa, matumizi ya koma na kikomo ni tofauti.

  • Iwapo sentensi inaanza na maelezo ya mnenaji, koma hufuata maelezo hayo nacho

kituo  huwekwa mwishoni mwa maneno

yanayonukuliwa k.m. Mwalimu aliniambia,

“Kiweke  kitabu  chako  mezani.”

  • Iwapo sentensi inaanza na maneno yanayonukuliwa, koma huwekwa 

mwishoni mwa maneno hayo nacho kituo.

huwekwa mwishoni mwa maelezo ya mnenaji k.m. “Kiweke kitabu chako 

mezani,”  mwalimu aliniambia.

  • Maelezo yanayofuata maneno yanayonukuliwa huanza kwa herufi ndogo  k.m. “Mkate huu  ni mtamu,” mtoto alisema.

  • Unapomnukuu mzungu mzaji, alama za kunukuu huwekwa baada ya kuweka koma,kituo,  kihisi,  kiulizi:

Sahihi makosa

  • Iwapo sentensi inaanza na maelezo ya mnenaji, koma hufuata maelezo hayo nacho kituo huwekwa mwishoni mwa maneno yanayonukuliwa k.m. Mwalimu aliniambia, “Kiweke kitabu chako mezani.”
  • Iwapo sentensi inaanza na maneno yanayonukuliwa, koma huwekwa mwishoni mwa maneno hayo nacho kituo huwekwa mwishoni mwa maelezo ya mnenaji k.m. “Kiweke kitabu chako mezani,” mwalimu aliniambia.
  • Maelezo yanayofuata maneno yanayonukuliwa huanza kwa herufi ndogo k.m.

“Mkate huu ni mtamu,” mtoto alisema.

Unapomnukuu mzungumzaji, alama za kunukuu huwekwa baada ya kuweka koma, kituo, kihisi, kiulizi: Sahihi makosa “--------------,” “--------------”,