Kinyume

- Kinyume ni sawa na “upande ule mwingine”.

- Kunavyo vinyume vya vitenzi na vya nomino.

 

Mifano:- 

Cheka (kitenzi); lia (kitenzi kinyume cha cheka);

 

Utajiri (nomino) – umaskini (nomino).

Kwa kawaida kuna njia kadhaa za kupata kinyume:

 • Kunyambua kitenzi

Baadhi ya vitenzi hunyambuliwa ili kupata kinyume chao k.m

vaa – vua, 

Ziba - zibua,

Tia - toa,

 

Muhimu

- Ni vyema uelewe mnyambuliko wa kitenzi kabla hujataja kinyume.

- Hii ni kwa sababu mnyambuliko wa vitenzi unaathiri hali ya kinyume k.m. tanda -tandua, tandika -tanduka, valia - vulia, valika - vulika

 

 • Jinsia ya kike au kiume k.m.

mwanamume – mwanamke,

mfarika – beberu,

kijakazi – kitwana n.k.

 

 •  Kinyume cha kimantiki k.m.

kasirika – furahi,

cheka – lia,

meza – tema,

uza – nunua,

giza – mwangaza,

usiku – mchana,

refu – fupi,

 

 •  Kinyume cha vitenzi visivyonyambuliwa k.m.

kimbia – tembea,

amka – lala,

tabasamu – nuna, • 2d570174-206a-42ef-b853-e15ef6620588 by https://tlcafrica.com/african_names.htm used under CC_BY-SA
 • 2e6827e9-b2ee-46e1-9699-b20628366d56 by blacknaija.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • kimbia by unknown & eLimu used under CC_BY-SA
 • refu by freemalaysiatoday.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • vaa by zmescience.com & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.