Matumizi ya 'na'

 

- 'na' hutumiwa kutolea maana mbalimbali katika sentensi. Kwa mfano,

 • -na- ya wakati uliopo

1. Tunasoma kwa bidii.

2. Mnaandika vizuri.

 

 • -na- ya kiunganishi

1. Juma na Fatuma ni wanafunzi hodari.

2. Kiswahili Teule na Uhondo wa Kiswahili ni vitabu vizuri.

 

 • -na- ya mnyambuliko – hali yakutendeana, kutendana.

1. Wao husaidiana kazini.

2. Sisi tunapendana sana.

 

 • -na- ya mtendaji

1. Chakula kilipikwa na shangazi.

 

2. Majeruhi walisaidiwa na wasamaria wema.

 

 •  -na- ya kumiliki.

1. Tuna vifaa vipya.

2. Ana kofia pana.

 

 • -na- ya ufupishaji na nafsi.

Nao waliamua kuondoka.

Naye alifurahia mwaliko huo.

 

 •  -na- ya hali.

1. Mwalimu ana furaha.

2. Mwanafunzi ana bidii.

 

 •  -na- ya uhusiano.

1. Nguo nazo ni safi.

2. Huko nako ni safi.

 

Zoezi

Chagua jibu sahihi la kuzikamilisha sentenzi hizi.


1. Kiatu ____ (nayo, nawe, nacho, nako) huvai kwa nini?

2. Mayai ____ (nazo,nayo, naye,nao) hutagwa na batamzinga.

3. Jua _____ (nayo, nalo, nacho, nao)  huwaka sana siku hizi.

4. Likizo ____ (nalo, nayo, nacho, naye) tumeanza leo.

5. Maiti ____ (naye, nayo, nazo, nawo) huzikwa kwa heshima.

6. Viumbe ____ (nao.nazo, nzvyo, naye) ni mali ya mungu.

7. Chumvi _____  (navyo, nacho, nazo, nao) hupatikana kila bahari.

8. Tabasamu ____ (nayo, nalo,nako, nacho) hufurahisha moyo.

9. Vita ____ (nayo,nazo, navyo, napo) huleta hasara kubwa.

10. Kuoga _____ (nayo,nalo,nazo, nako) hufaa kila siku. • na_1 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_2 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_3 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_4 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_5 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_6 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.