Ritifaa

Ritifaa ( ʻ )

Hutumika:

  • Katika maneno yenye ving’ong’o k.m ng’ombe, ng’oa n.k. Ritifaa huwekwa juu baada ya herufi g k.m ng’ombe.

Mifano:

Ning’inia, ng’amua, ng’ambo, ng’onda, ng’ang’ania, kung’ara ...

  • Kwenye shairi kuonyesha kuwa herufi fulani imeachwa. k.m. ‘shasikia mametu amefika salama.

Zoezi

Katika sentensi zifuatazo, weka alama za ritifaa katika maneno yanayostahili. 

1. Alishangaa na kubungaa kutokana na habari hizo.

2. Ngoja ngoja yake ilituchelewesha kungoa nanga.

3. Nguo hiyo ilingara sana.

4. Ameamua kuenda ngambo.

5. Kiongozi huyo ameamua kungoka madarakani.

6. Ngombe wa mjomba alipelekwa malishoni.

7. Shangwe na vigelegele vilisikika walipongamua kuwa wameshinda.

8.  Maskini mtoto huyo alingangania chakula licha ya kukonda kama ngonda. 

9. Alimpiga ngumi usoni. 

10. Baba alimchinja ngonzi wake na kuuza ngozi.