Ngeli ya MU - MU

- Ngeli ya MU huonyesha HUMU, HUMO, MLE, ambamo ni ndani. Kwa mfano: Chumbani, shimoni, nyumbani, ama mafichoni.

 

- Viarifu vya ngeli hii huanza kwa silabi mu ndiposa inaitwa ngeli ya mahali ya mu-mu k.m. Sokoni mmejaa wauzaji.

  • Vivumishi Nomino za mahali hubaki vivyo hivyo katika umoja na wingi. Kwa hivyo, vivumishi vyake ni katika hali moja tu.
  • Kiwakilishi amba- Sakafuni ambamo anafagia munateleza.

N/B Jina lolote linaweza kupachikwa kiambishi tamati -ni, nalo likawa au likageuka kuwa mahali HUMU, HUMO, MLE. 

Mifano: 

a) Maskanini humu mna Bi. Harusi.

b) Maskanini humo mna Bi. Harusi.

c) Maskanini mle mna Bi. Harusi.

 

1.  'O' rejeshi

Sakafuni anamofagia munateleza.

2. Ndi- ya kusisitiza

Hamamuni alimoogea ndimo humu.

3. Si- ya kukataa

Hamamuni alimoogea simo humu.

4. Na- ya kirejelei

Humu namo muna watoto wengi.

5. Viashiria/vionyeshi

humu humo mle

  • Viashiria/vionyeshi visisitizi.

mumu humu, mumo humo, mle mle.

  • Viashiria/vionyeshi radidi.

humu humu, humo humo, mle mle.

6. Kivumishi -enye.

Sokoni mwenye wateja muna kelele.

7. Kivumishi -enyewe.

Tuliogelea mtoni mwenyewe.

8. Kivumishi -ote.

Mezani mote muna vitabu.

9. Kivumishi -o-ote.

Nitakaa momote nitakamoonyeshwa.

10. Kivumishi -ngi.

Hotelini mwingi muna starehe.

11. Kivumishi -ngine.

Amehamia mjini mwingine.

12. Kiulizi –pi?

Mjomba alienda shuleni mupi?