Ngeli ya KI - VI

- Ngeli hii hujumuisha aina tatu za nomino:

1. Nomino zote (ziwe za viumbe au vitu) katika hali ya udogo k.m: kitoto,kijito, kijitu, kijia, kigombe n.k.

2. Nomino za vitu ambazo umoja huanza kwa silabi ch na wingi huanza kwa vy k.m: chakula, chombo, cherehani, chuo, chandarua.

3. Nomino za vitu ambazo katika hali ya wastani, umoja huanza kwa silabi ki na wingi huanza kwa silabi vi k.m. kiti, kikapu, kioo, kisigino, kikombe n.k.

 

Vivumishi Kiwakilishi amba–

  • Umoja: Kioo ambacho alikinunua ni kikubwa.
  • Wingi: Vioo ambavyo walivinunua ni vikubwa.

'O' rejeshi

  • Umoja: Kioo alichokinunua ni kikubwa.
  • Wingi: Vioo walivyovinunua ni vikubwa.

Ndi- ya kusisitiza

  • Umoja: Kikapu hiki ndicho alichokinunua.
  • Wingi : Vikapu hivi ndivyo walivyovinunua.

Si- ya kukataa

  • Umoja: Kikapu hiki sicho alichokinunua.
  • Wingi: Vikapu hivi sivyo walivyovinunua.

Na- ya kirejelei

  • Umoja: Chumba hicho nacho hakikaliki. Kinalo joto jingi.
  • Wingi : Vyumba hivyo navyo havikaliki. Vinalo joto jingi.

Viashiria/vionyeshi

  • Umoja: hiki hicho kile
  • Wingi: hivi hivyo vile

 

Viashiria/vionyeshe visisitizi

  • Umoja: kiki hiki chicho hicho kile kile,
  • Wingi: vivi hivi vivyo hivyo vile vile

Viashiria/vionyeshi radidi

  • Umoja: hiki hiki hicho hicho kile kile
  • Wingi: hivi hivi hivyo hivyo vile vile

Kivumishi -enye

  • Umoja: Kikombe chenye maziwa kimeletwa.
  • Wingi: Vikombe vyenye maziwa vimeletwa.

Kivumishi -enyewe.

  • Umoja: Kitoto kilikula chenyewe.
  • Wingi: Vitoto vilikula vyenyewe.

 

Kivumishi -ote

  • Umoja: Amekisoma kitabu chote.
  • Wingi: Wamevisoma vitabu vyote.

Kivumishi -o-ote

  • Umoja: Mshona nguo atakitumia cherehani chochote.
  • Wingi : Washona nguo watavitumia vyerehani vyovyote.

Kivumishi -ngi

  • Umoja: Mpishi alinipikia chakula kingi.
  • Wingi: Wapishi walitupikia vyakula vingi.

Kivumishi -ngine

  • Umoja: Mpishi alinipikia chakula kingine.
  • Wingi: Wapishi walitupikia vyakula vingine.

 

Vivumishi vya idadi

kimoja, viwili, vitatu, vinne, vitano, sita, saba, vinane, tisa, kumi, kumi na kimoja, kumi na viwili n.k

Kiulizi -pi?

Umoja: Atakitumia kisu kipi kukatia?

Wingi: Watavitumia visu vipi kukatia?

 

Kiulizi -ngapi?

  • Wingi : Watoto walitumia vichana vingapi kuchania?
  • Jikumbushe: Je, tulisema nini kuhusu ngapi katika hali ya umoja?

 

Muhimu

1. Ngeli tatu tu ndizo zina nomino za viumbe vilivyo na uhai: a) A-WA: hali ya wastani; b) KI-VI: hali ya udogo; c) LI-YA: hali ya ukubwa

2. Nomino yoyote inapokuwa katika hali ya udogo huhamia katika ngeli ya KI-VI

3. Nomino yoyote ikigeuzwa na kuwa katika hali ya ukubwa huihama ngeli ya hapo awali na kuingia ile ya LI-YA



  • kitoto1 by https://en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • kikapu_1 by basket.kde.org eLimu used under CC_BY-SA
  • f_f by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • g_r by www.6minutes.com.au & eLimu used under CC_BY-SA
  • jf2 by linkedin.com& eLimu used under CC_BY-SA
  • jkjk by mamabee.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • kkk1_1 by www.khmerbit.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • kisu_1 by healthyhomeandkitchen.com & eLimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.