Ngeli ya LI - YA

Ngeli ya LI-YA

Ngeli hii huwa na aina tatu za nomino

 1. . Nomino zote katika hali ya ukubwa k.m. jitu, toto, jia, buzi, gombe, lango, jumba, jito n.k.
 2.  Nomino za vitu ambazo katika hali ya umoja huchukua viambishi mbalimbali lakini wingi huchukua kiambishi ma- k.m gari -magari, swali -maswali, jicho -macho, vumbi – mavumbi
 3.  Nomino za vitu ambazo katika hali ya umoja huchukua viambishi mbalimbali lakini wingi huchukua kiambishi m e k.m. jino – meno

 • Vivumishi Kiwakilishi amba- Umoja: Tunda ambalo anakula halijaiva. Wingi: Matunda ambayo wanakula hayajaiva.

 • 'O' rejeshi Umoja: Tunda analokula halijaiva. Wingi: Matunda wanayokula hayajaiva.
 • Ndi- ya kusisitiza Umoja: Jizi hili ndilo lililonishambulia. Wingi: Majizi haya ndiyo yaliyotushambulia.

 • Si- ya kukataa Umoja: Jizi hili silo lililotoroka. Wingi: Majizi haya siyo yaliyotoroka.
 • Na- ya kirejelei Umoja: Jino hili nalo limeniuma kwa siku nyingi. Wingi: Meno haya nayo yametuuma kwa siku nyingi.

 • Viashiria/vionyeshi Umoja: hili hilo lile Wingi: haya hayo yale.
 • Viashiria/vionyeshi visisitizi Umoja: lili hili lilo hilo lile lile Wingi: yaya haya yayo hayo yale yale.
 • Viashiria/vionyeshi radidi Umoja: hili hili hilo hilo lile lile Wingi: haya haya hayo hayo yale yale.

 • Kivumishi -enye Umoja: Gari lenye hitilafu ya mtambo ni hatari kusafiria. Wingi: Magari yenye hitilafu za mitambo ni hatari kusafiria.

 • Kivumishi -enyewe Umoja: Tawi limevunjika lenyewe. Wingi: Matawi yamevunjika yenyewe.
 • Kivumishi -ote Hutumika kuonyeshea ukamilifu wa kila sehemu k.m Darasa lote limefurika. Umoja: Darasa lote limepambika. Wingi: Madarasa yote yamepambika.

 • Kivumishi -o-ote Umoja: Mpishi atalitumia jiko lolote litakalopatikana. Wingi: Wapishi watayatumia majiko yoyote yatakayopatikana.
 • Kivumishi -ngi Umoja: Uwanjani hakuna vumbi jingi. Wingi: Uwanjani hakuna mavumbi mengi.

Muhimu Kivumishi jingi hutumika kwa nomino chache tu katika ngeli hii ya LI-YA. k.m vumbi, tunda, gari n.k.

 • Kivumishi -ngine Umoja: Nitalijibu swali jingine iwapo nitaulizwa. Wingi:
 • Tutayajibu maswali mengine iwapo tutaulizwa. Kiulizi -pi? Umoja: Baba alilitumia gari lipi? Wingi: Akina baba waliyatumia magari yapi?

Kiulizi -ngapi Wingi: Wasafiri waliyatumia magari mangapi? • jino2 by Clipart panda used under CC_BY-SA
 • Jizi by The 7s blog used under CC_BY-SA
 • Magari by Houston Chronicle used under CC_BY-SA
 • Tunda by My adalaide used under CC_BY-SA
 • Viashiria by Ron Paul forums used under CC_BY-SA
 • Madarasa by Gerakan Sekolah used under CC_BY-SA
 • Magari by Houston Chronicle used under CC_BY-SA
 • Uwanjani by Mail online used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.