Kistari kifupi

Kistari kifupi ( - )

Hutumika:

  • Kuonyesha mzizi wa neno k.m. -zuri, -baya, -erevu.
  • Kuendeleza neno linapokatwa katika sentensi mwishoni mwa mstari k.m Kitabu chenyewe kili- gharimu pesa nyingi. Somo la Jiografia lina- pendeza wanafunzi wengi.
  •  Kusisitiza sauti k.m Walimcheka ha-ha-ha kwa ujuha wake.

  • Kuunganisha tarakimu kuonyesha mwanzo hadi mwisho k.m Alikuwa mkurugenzi mkuu 1991 - 2006. v) Alifunza Kiswahili Januari - Oktoba. Katika uandishi wa tarehe k.m. 7 - 4 - 2006.