Ngeli ya KU - KU

- Ngeli ya KU huonyesha mahali HUKU, HUKO, KULE, ambako ni mahali kusiko dhahiri au wazi; si maalum hata kama ni karibu nasi. 

- Ngeli hii hujumuisha aina mbili za maneno. 

• Nomino za mahali. 

• Vitenzi vinavyoanza kwa silabi ku. 

 

N/B Jina lolote linaweza kupachikwa kiambishi tamati -ni, nalo likawa au likageuka kuwa mahali HUKU, HUKO, KULE. 

Mifano: 

a) Nyumbani huku kunapendeza.

b) Nyumbani huko kunapendeza.

c) Nyumbani kule hakupendezi.

Vivumishi

1. Kiwakilishi amba- 

Kucheka ambako anacheka kunapendeza. 
Machimboni ambako kunachimbwa hakuna mawe imara. 

2. “O” rejeshi

Kucheka anakocheka kunapendeza.
Machimboni kunakochimbwa kuna mawe imara.

3. Ndi- ya kusisitiza

Kuogelea ndiko kulikonichelewesha.
Nyumbani kwa Musa ndiko kule.

4. Si- ya kukataa

Kuogelea siko kulikonichelewesha.+
Nyumbani kwa Musa siko kule.

5. Na- ya kirejelei

Kibandani huku nako kuna vimelea wengi. 
Kusoma nako kuna faida.

6. Viashiria/vionyeshi: a) huku, b) huko, c) kule. 

- Viashiria/vionyeshi visisitizi: kuku huku,  kuko huko,  kule kule.
- Viashiria/vionyeshi radidi: huku huku, huko huko, kile kile. 

7. Kivumishi -enye 

Kushirikiana kwenye manufaa kunapendeza. 
Mtoni kwenye samaki huvutia wavuvi. 

8. Kivumishi -enyewe. 

Kuogelea kwenyewe kulichosha.
Mtoni kwenyewe hakuna samaki wengi.

 

9. Kivumishi -ote

Mezani kote kuna vitabu.
Kujibidiisha kwao kote hakukuwawezesha washinde.

10. Kivumishi -o-ote

Nitakaa kokote nitakakoonyeshwa.
Hatutashiriki kucheza kokote kule.

11. Kivumishi -ngi

Kulalamika kwingi hakufai.
Hotelini kwingi kumejaa watalii.


12. Kivumishi -ngine

Kuvaa kwingine kunaaibisha.
Viwanjani kwingine hakukuwa na michezo.

13. Kiulizi -pi?

Ni kusoma kupi kulikotuzwa?

 

Muhimu

Kwa vyovyote vile usichanganye vivumishi vya ngeli hizo tatu za mahali. Kwa kawaida vivumishi vya: 

  • M U - M U huwa na herufi m k.m. Nyumbani ambamo munasafishwa hamupendezi. 
  • PA–PA huwa na herufi p k.m. Nyumbani ambapo panasafishwa hapapendezi. 
  • K U - K U huwa na herufi k k.m. Nyumbani ambako kunasafishwa hakupendezi.