Ngeli ya U - U

Ngeli hii hujumuisha nomino za aina mbili.

  • Nomino za vitu visivyohesabika wala kugawika, visivyo na umoja wala wingi – huanza kwa u au w k.m. uji, ugali, ujima, ugoro.

  • Nomino za maneno ya dhahania (yaani maneno yanayoonyesha hali ya jambo au kitu). Kwa kawaida maneno haya huanza kwa u au w k.m. woga, umaskini, uzembe, urafiki, wivu, werevu, ujinga, uasi n.k.

Umoja na wingi

- Wema huu ulimfaidi. Wema huu uliwafaidi.

- Ujanja huo ulimponya. Ujanja huo uliwaponya.

- Unga ule ulikuwa mweupe. Unga ule ulikuwa mweupe

Vivumishi -Vivumishi vya ngeli hii ni sawa na vile vya ngeli ya U - ZI (hali ya umoja).

Matumizi ya viambishi katika ngeli ya U - U

1) Viambishingeli (u - u)

i) Wino wangu umemwagika.   -   Wino wetu umemwangika.

ii) Uhuru wa nchi hii umekomaa.   -   Uhuru wa nchi hizi umekomaa.

 

2) Kirejeshi - O (o - o)

i) Uji uliomshibisha mtoto ni huo.   -   Uji uliowashibisha watoto ni huo

ii) Ukimwi ambao unamwangamiza mtu ni hatari.   -   Ukimwi ambao unawaangamiza watu ni hatari.

 

3) Kiunganifu: "-A" (wa - wa)

i) Upupu wa hapa uliniwasha.   -   Upupu wa hapa ulituwasha.

ii) Upanzi wa mti ni jukumu muhimu.   -   Upanzi wa miti ni majukumu muhimu.

 

4) Sifa -enye, -enyewe; (we - we)

i) Ujanja wenye wasiwasi uwache.   -   Ujanja wenye wasiwasi mwache.

ii) Ugoro wenyewe umeniudhi.   -   Ugoro wenyewe umetuudhi

 

5) Sifa -ote, -o-ote (wo - wo)

i) Wasiwasi wake wote umeisha.   -   Wasiwasi wao wote umeisha.

ii) Wizi wowote hauna nafasi kwangu.   -   Wizi wowote hauna nafasi kwetu.

 

6) Sifa -ngi, -ingine n.k. (mwi - mwi)

i) Unga wangu mweupe si mweupe.   -   Unga wetu mweupe si mweusi.

ii) Uyoga mwembamba ni wako.   -   Uyoga mwembamba ni wetu.