Nomino ambata

Miundo ya nomino ambata

Nomino ambata hupatikana baada ya kuyashikanisha maneo mawili au zaidi ili kutoa maana fulani k.m. mwanahewa. 

Nomino za aina hii huandikwa likiwa neno moja, mfano kitozamachozi. Vilevile, huweza kutenganishwa kwa vistari vifupi, mfano isimu-jamii. Nomino ambata zina miundo ifuatavyo:

 

a) Nomino na nomino. 

Hizi ni nomimo ambata zinazotokea kwa kuunganisha nomino mbili.

Mifano:

mwanasoka - mwana + soka

gugumaji - gugu + maji,

batamzinga - bata + mzinga,

mbwamwitu - mbwa + mwitu.

askarikanga - askari + kanga.

 

b) Nomino zaidi ya mbili.

Nomino ambata zinazoundwa kwa kuunganisha nomino zaidi ya mbili. 

Mfano:

mwanaelimusiha - mwana + elimu + siha.

mwanasarufimuundo - mwana + sarufi + muundo.

 

c) Nomino na kitenzi. 

Nomino ambata zinazoundwa kwa kuunganisha nomino na kitenzi.

Kwa mfano:Bbongolala - bongo + lala, hatimiliki - hati + miliki, mamapima - mama + pima.

 

d) Nomino na kivumishi. 

Huundwa kwa kuunganisha nomino na kivumishi.

Mifano ni pembetatu - pembe + tatu, duaradufu - duara + dufu, malighafi - mali + ghafi, mjamzito - mja + mzito.

 

e) Nomino na kielezi. 

Mfano: kipaumbele - kipau + mbele, (kipewacho umbele).

 

f) Kitenzi na nomino. 

Mfano, chemshabongo - chemsha + bongo.

 

g) Kitenzi na kitenzi. 

Mifano: pandashuka - panda + shuka, patashika pata + shika.

 

h) Kitenzi na nomino.

Mfano, chemshabongo - chemsha + bongo.

 

i) Kitenzi na kitenzi. 

Mifano: pandashuka - panda + shuka, patashika - pata + shika.

 

Mifano kwa muhtasari

mwana + nchi  -  mwananchi.

mwana + muziki  -  mwanamuziki.

mwana + siasa - mwanasiasa.

mwana + haramu - mwanaharamu.

mwana + sheria - mwanasheria.

mwana + mke - mwanamke.

askari + jela = askarikanzu

mwana + mkiwa = mwanamkiwa

mbwa + mwitu = mbwamwitu

pembe + tatu = pembetatu

kiinua + mgongo = kiinuamgongo

nusu + kipenyo = nusukipenyo

simba + marara = simbamarara