Ukubwa na udogo

A. Ukubwa

Kuna kanuni zinazofuatwa ili kubadilisha nomino kuwa katika hali ya ukubwa. Kwa mfano:

a) Jamii ya nomino zenye kianzo ki katika hali ya kawaida, huweza kugeuzwa katika ukubwa kwa kudondosha ki na kupachika ji. 

Mifano:

kichwa - jichwa

kisima - jisima

kivuli - jivuli

 

b) Aina fulani ya nomino zinazoundwa au zinazotokana na silabi mbili, huweza kukubakika kudondosha silabi awali na kuambatisha ji kupata ukubwa.

Mifano:

mti - jiti

mwana - jana

mwehu - jehu

mfu - jifu

 

c) Kundi la nomino zinazoanza kwa ji hupachikwa ji tena ili kuunda ukubwa:

Mifano:

jina - jijina

jipu - jijipu

jitimai - jijitimai

jifya - jijifya

 

d) Nomino zozote zisizokuwa na mpangilio maalum wa vianzio vya viambishi jina huweza kupachikwa ji mwanzoni ili kupata ukubwa.

Mifano:

taa - jitaa

sahani - jisahani

redio - jiredio

shwa katika halimeza - jimeza

 

e) Nomino nyingine zinaweza kubadilishwa katika hali ya ukubwa baada ya kudondosha herufi ya mwanzo ya  kianziojina. Aghalabu herufi zinazodondoshwa ni m au u endapo nomino hizo zinaanzia kwa: mb-, nd-, nj-, ng-

Mifano:

ngazi - gazi

ngamia - gamia

mbuga - buga

mbalamwezi - balamwezi

 

f) Jinsi nyingine ya kupata ukubwa ni kudondosha herufi ya mwanzo m katika nomino zozote zenye  miundo au maumbo ya silabi tatu au zaidi zinazoanza kwa herufi m.

mlolongo - lolongo

mfereji - fereji

msumeno - sumeno

mguu - guu

Kumbuka majina yote ya ukubwa huorodhesha katika ngeli ya LI- YA. Kwa hivyo basi, jina lolote la ukubwa wingi wake huanza kwa silabi ma.

Mifano:

jijipu - majijipu

jitu - majitu

Domo - madomo

Doo - madoo 

Sentensi za wastani na ukubwa

B. Udogo 

Hali ya udogo hupatikana kwa urahisi baada ya kupata ukubwa . Ukitaka kupata usogo wa nomino yoyote, utapachika ki mwanzo wa nomino ya ukubwa. Kwa hivyo: Ki + UKUBWA = UDOGO

Tazama:

Ukubwa        udogo

jichwa           kijichwa

jitu                 kijitu

toto                kitoto

lango            kilango

Kumbuka nomino zote za hali ya udogo huorodheshwa katika ngeli ya KI - VI.

Sentensi za ukubwa na udogo

 

Zoezi

Fuata maagizo ili ubadilishe sentensi hizi katika hali uliyoagizwa kufuata

1. Mbwa mkubwa alimkibia ng'ombe.  ( andika katika ukubwa)

2. Kijoka kilichokiuma kibuzi ni hiki.  ( andika katika wingi)

3. Watoto wale ni wadogo. ( andika katika ukubwa)

4. Milima yote haina miti mingi ( andika katika udogo)

5. Mtoto yule mdogo ni wa mgeni wangu. (andika katika udogo/wingi)