Ngeli ya U - I

- Ngeli hii hujumuisha nomino za vitu visivyo na roho ambazo umoja huchukua viambishi m na wingi huchukua viambishi mi

k.m mti – miti, mto – mito, mlima – milima, mguu – miguu, mtetemeko – mitetemeko. n.k.

 

 • Vivumishi Kiwakilishi amba-

Umoja: Mto ambao ulifurika sasa umekupwa. Wingi: Mito ambayo ilifurika sasa imekupwa.

 • 'O' rejeshi

Umoja: Mto uliofurika sasa umekupwa. Wingi: Mito iliyofurika sasa imekupwa.

 • Ndi- ya kusisitiza

Umoja: Mkeka uliosafishwa ndio huo. Wingi: Mikeka iliyosafishwa ndiyo hiyo.

 • Si- ya kukataa

Umoja: Mkeka uliosafishwa sio huo. Wingi: Mikeka iliyosafishwa siyo hiyo.

 • Na- ya kirejelei

Umoja: Mkono wangu nao umepona. Wingi: Mikono yetu nayo imepona.

 • Viashiria/vionyeshe

Umoja: huu huo ule Wingi: hii hiyo ile Viashiria/vionyeshei visisitizi Umoja: uu huu uo huo ule ule Wingi: ii hii yiyo hiyo ile ile

 • Viashiria vionyeshi radidi

Umoja: huu huu huo huo ule ule Wingi: hii hii hiyo hiyo ile ile

 • Kivumishi -enye

Umoja: Mgodi wenye almasi umefunguliwa. Wingi : Migodi yenye almasi imefunguliwa.

 • Kivumishi -enyewe

Umoja: Mti umeanguka wenyewe. Wingi: Miti imeanguka yenyewe.

 • Kivumishi -ote

Umoja: Msitu wote umezungushwa ukuta. Wingi: Misitu yote imezungushwa kuta.

 • Kivumishi -o–ote

Umoja: Nitautumia mchi wowote. Wingi: Tutaitumia michi yoyote.

 • Kivumishi -ngi

Wingi: Tuliichimba mitaro mingi.

Jikumbushe: Je, ulijifunza nini kuhusu kivumishi -ngi katika hali ya umoja?

 • Kivumishi -ngine.

Umoja: Mtoto alinunuliwa mpira mwingine. Wingi: Watoto walinunuliwa mipira mingine.

 • Kiulizi -pi?

Umoja: Gari lilienda kwa mwendo upi? Wingi: Magari yalienda kwa miendo ipi? Kiulizi -ngapi? Wingi: Mama alinunua miwa mingapi?

Vivumishi vya idadi mmoja, miwili, mitatu, minne, mitano, sita, saba, minane, tisa, kumi, kumi na mmoja, kumi na miwili n.k • q1_2 by popscreen.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • q2_2 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • q3_2 by council.providenceri.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • q4_3 by fifchristian.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • q5_3 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • q6_1 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.