Nomino katika hali tofauti

Nomino katika hali tofauti

Nomino za Kiswahili huwa katika hali tatu: wastani, udogo na ukubwa

Hali ya wastani Hali ya wastani ni hali ya kawaida. Wengine husema hali ya katikati. Katika hali hii, nomino huwa katikati. Si kubwa wala si ndogo. Aghalabu, nomino nyingi hutumiwa katika hali hii. Kwa mfano mtu, njia, ng’ombe, gari, mtoto, mti, kikapu n.k. Nomino katika hali ya wastani huwa katika ngeli mbalimbali kulingana na uwiano wa kisarufi.

Hali ya udogo Nomino huwa katika hali ya udogo inapodunishwa. Kudunishwa ni kufanywa iwe duni au ndogo k.m. mtu -kijitu, njia •kijia, ng’ombe - kigombe, gari - kigari, mtoto -kitoto, mti - kijiti, kikapu - kijikapu.

Nomino inapodunishwa, mabadiliko fulani hutokea

  • Kiambishi cha nomino hiyo huwa ni ki (umoja) na vi (wingi). Nomino hiyo huingia katika ngeli ya ki-vi. k.m. Mtu amefika – kijitu kimefika; Watu wamefika – Vijitu vimefika.
  •  Baadhi ya nomino huongezewa silabi ji:

a) Nomino ambazo katika hali ya wastani zilikuwa na silabi mbili k.m. mtu – kijitu, mto – kijito

b) Nomino ambazo katika hali ya wastani zilikuwa katika ngeli ya KI - VI. Nomino hizi huongezewa silabi ji bila kuzingatia idadi ya silabi. k.m. kikapu – kij ikapu, kikombe – kijikombe

c) Nomino ambazo hupatikana katika ngeli ya LI-YA katika hali ya kawaida k.m. darasa – kijidarasa, tunda - kijitunda

  • Baadhi ya nomino, hususan zile ambazo katika hali ya wastani hazipo katika ngeli ya LI-YA na KI-VI, huondolewa herufi ya kwanza, kabla ya kuweka kiambishi ki k.m. njia – kijia, ng’ombe – kigombe, mtu – kijitu, mbwa – kijibwa, nguo – kiguo, nyumba – kijumba,

Hali ya ukubwa Nomino huwa katika hali ya ukubwa inapofanywa kuwa kubwa k.m mtu - jitu, njia -jia, ng’ombe - gombe, gari - jigari, mtoto - toto, mti - jiti, kikapu - kapu/jikapu. Nomino zote katika hali ya ukubwa huwa katika ngeli ya LI-YA.

Nomino inapofanywa kubwa na kuchukua hali ya ukubwa, mabadiliko fulani hutokea.

  • Herufi ya kwanza huondolewa k.m. njia – jia, ngoma – goma, mbuzi – buzi, mtoto – toto, mguu – guu, nguo – guo, mkono – kono, ufagio – fagio, upanga – panga, ufunguo – funguo.
  • Silabi j i huongezwa katika nomino ambazo: i) katika hali ya wastani zilikuwa katika ngeli ya LI-YA k.m. gari – jigari, darasa – jidarasa ii) katika hali ya wastani zina silabi mbili pekee k.m. mtu – jitu

Tazama jedwali lifuatalo

Udogo Wastani Ukubwa kidomo mdomo domo kijikiti kiti jikiti kijijicho jicho jijicho kijijiko kijiko jijiko kijisichana msichana jisichana kikuta ukuta kuta kilango mlango lango kijibuyu kibuyu jibuyu kibuzi mbuzi buzi kijisu kisu jisu.

Udogo                   Wastani           Ukubwa

Kidomo              mdomo           domo

Kijikiti               kiti                 jikiti

Kijijicho             jicho               jijicho

Kijijiko              jiko                jijiko

Kijischana          msichana         jischana

Kikuta              ukuta              kuta

Kilango             mlango           lango

Kijibuyu            kibuyu             jibuyu

Kibuzi              mbuzi              buzi

Kijisu               kisu                jisu