Kistari kirefu

Kistari kirefu ( – )

Pia huitwa deshi.

Hutumika:

  • Kuunganisha sentesi mbili ikiwa sentensi ya pili inafafanua sentensi ile ya kwanza. K.m. Wageni walikuwa na tabia nzuri - unyenyekevu na heshima. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na waja wengi - wazee kwa vijana.
  • Kutoa maelezo zaidi. k.m. Wachezaji machachari - Kamau, Mwazemba na Muholo - walifika uwanjani mapema.
  • Katika kuandika orodha. K.m Kitabu cha Kiswahili kimegawanywa katika sehemu tano: - Kusoma - Kusikiliza na kuongea - Sarufi - Msamiati - Kuandika.