Usemi wa taarifa

Usemi wa taarifa

Pia huitwa usemi kuripoti. Hutumika katika kuripoti yale yaliyosemwa na mzungumzaji bila kunukuu maneno yake moja kwa moja.

Kwa hivyo:

  • Alama za kunukuu hazitumiki.
  • Alama za kuulizia hazitumiki.
  • Alama za hisi hazitumiki.
  • Kwa kawaida wakati uliopita hutumika.
  • Viashiria vya kwanza hubadilika na kuwa vya pili au vya tatu k.m. “ Mwanafunzi huyu ni mtiifu,” mwalimu alisema. Mwalimu alisema kuwa mwanafunzi huyo/yule alikuwa mtiifu.
  • Nafsi ya kwanza na pili hubadilika na kuwa ya tatu. k.m. “Mimi ninasoma kwa bidii,” mtoto alisema. Mtoto alisema kuwa yeye alisoma kwa bidii.

  • Viwakilishi vya nafsi ya kwanza na ya pili hubadilika na kuwa vya nafsi ya tatu. “ Nitaandika insha ya kupendeza,” mwanafunzi aliahidi. Mwanafunzi aliahidi kuwa angeandika insha ya kupendeza.

“Ukisoma kwa bidii utafua dafu,” mvyele alimshauri mwanawe. Mvyele alimshauri mwanawe kuwa iwapo a n g esoma kwa bidii angefua dafu.

  •  Vimiliki vya nafsi ya kwanza na ya pili hubadilika na kuwa vimiliki vya nafsi ya tatu. k.m. “Kitabu changu ni kipya,” mtoto alisema. Mtoto alisema kuwa kitabu chake kilikuwa kipya.

  •  “ - t a - ” ya wakati ujao hubadilika na kuwa -nge-. “Nitaondoka kuelekea ughaibuni,” shangazi alisema. shangazi alisema angeondoka kuelekea ughaibuni.Ki-ya masharti hubadilika na kuwa -nge-k.m. “Ukisoma kwa bidii utafua dafu,” mama alimweleza mwanawe. Mama alimweleza mwanawe kuwa iwapo angesoma kwa bidii angefua dafu.
  • Sasa hubadilika na kuwa wakati huo/ule. k.m “Nitaondoka sasa” mgeni alisema. Mgeni alisema angeondoka wakati huo/ule.
  •  Leo huwa siku hiyo. k.m. “Tutacheza leo uwanjani,” wanafunzi walisema. Wanafunzi walisema kuwa wangecheza siku hiyo/ile uwanjani.

  • Kesho huwa siku iliyofuata. k.m. “Nitaenda sokoni kesho,” mjakazi alisema. Mjakazi alisema kuwa angeenda sokoni siku iliyofuata.

  •  Jana huwa siku iliyotangulia/iliyopita. k.m. “Tulinyeshewa sana jana,” wasafiri walisema. Wasafiri walisema kuwa siku iliyotangulia/ iliyopita walinyeshewa sana.

  • Viulizi na vihisi havitumiki. k.m. “Kwa nini ulichelewa?” mwalimu alimwuliza mwanafunzi. Mwalimu alitaka kujua sababu ya kuchelewa kwa mwanafunzi. “Lo! Kumbe ni mtoto!” Mama alishangaa’ Mama alishangaa kuwa huyo alikuwa ni mtoto.Matumizi ya “ni” Silabi  ni ina  matumizi mbalimbali.



  • usemi_tarifa_1 by wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • usem_4 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • usemi_2 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • usemi_3 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • usemi_6 by marketplace.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • usemi_7 by tindonkey.com & eLimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.