Matumizi ya 'kwa'

 

'Kwa' ina matumizi mbalimbali.

 • Kwa ya kuonyeshea kuwa chombo kinatumika kufanyia kazi. Huonyesha uhusiano kati ya tendo na kitu kilichotumika, (Kwa ya matumizi). k.m.

- Mkulima anapalilia kwa jembe.

- Baina alimgonga kwa fimbo. 

 

 •  Kwa ya uhusiano wa mtu/watu na mahali k.m.  (Kumhusu mtu fulani). k.m.

- Mtoto huyu anatoka kwa Njoroge.

- Ninaenda kwa daktari.

 

 •  Kwa ya pamoja k.m.

Wazee kwa vijana walihudhuria mkutano huo.

 

 • Kwa ya hali (kielezi).  k.m.

- Tulienda moja kwa moja hadi darasani.

- Walikuwa kwa haraka walipotupitia.

 

Pia huonyesha jinsi au namna jambo lilivyotendwa.

- Mwalimu alitukaribisha kwake kwa unyenyekevu.

- Bi. Salim alitueleza jambo hilo kwa ufupi. (kwa ufupi - inajibu swali aje? au vipi?).

 

 •  Kwa ya kuonyeshea sehemu, kama vile katika aksami.

- Mwanafunzi amepata maksi sabini kwa mia moja.

 

 • Kwa ya unganifu - hutumika kwa vitenzi vilivyo na viambishi ku na nomino za mahali k.m.

- Kucheza kwa Susana kulifurahisha wengi.

- Nyumbani kwa mjomba ni paradiso.

 • Kwa ya kiulizi na kwa ya kujibia k.m.

- Mwalimu Tobias: Kwa nini umechelewa?

- Kongole: Kwa sababu nilianguka.

 

 • Kwa ya nia/lengo au sababu k.m.

- Nitafika kwa kumwona; Walikuja kwa harusi.

 

 • Kwa ya kimiliki cha nafsi ya kwanza (umoja) katika ngeli ya KU-KU. k.m.

- Kusoma kwangu kunanifaa.

- Chumbani kwangu hakukaliki.

 

Eleza matumizi ya 'kwa' katika sentensi zifuatavyo.

1. Shangazi alitushukuru kwa kujitolea kwetu.  

2. Babu ni kibogoyo, yeye anakula wali kwa mchuzi.

3. Kwa Daladala kunapendeza mno. 

4. Tulitumia fedha zetu zote kwa sababu ya ajali iliyotupata.

5. Kwa (a) mara ya kwanza, macho yangu yalimwona nyanguni, ana kwa (b) ana.

  • kwa_1 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • kwa_2 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • kwa_3 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • kwa_70 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • kwa_jembe by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.