Nomino

Nomino

 • Nomino ni neno linalotaja jina la mahali, kiumbe, kitu, au hali. Pia huitwa jina au nauni. k.m. sokoni, kikombe, punda, werevu n.k.
 • Uundaji wa nomino kutokana na vitenzi. Mtu atendapo kitendo, bila shaka kunakuwa na matokeo. Matokeo hayo huwa ni nomino k.m. Nikikimbia (kitenzi) matokeo huwa ni mbio (nomino).

Nomino kutokana na sifa Sifa ni neno ambalo huelezea mengi kuhusiana na nomino. Sifa hiyo inaweza kutoa nomino ambayo ni jina linalotaja sifa yenyewe k.m kubwa – ukubwa.

Tazama mifano ifuatayo:

 • Sifa Nomino kutokana na sifa

refu urefu -geni ugeni -zuri uzuri -baya ubaya -gumu ugumu -chungu uchungu -ema wema -eupe weupe -nene unene -pya upya

 • Sifa kutokana na vitenzi

Sifa zinaweza kuundwa kutokana na vitenzi. k.m Mtoto mtiifu hutii wakubwa wake. sifa kitenzi Mgeni mnyamavu alinyamaza sana. sifa kitenzi

Tazama mifano ifuatayo:

 • Kitenzi Sifa soma msomaji ogopa mwoga iba mwizi chora mchoraji asi mwasi pika mpishi linda mlinzi suka msusi chokoza mchokozi jenga mjenzi • df by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • xc by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • DC by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • FB by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.