Insha ya ajali ya moto

 

Mambo ya kuzingatia:

  • Moto ulizuka wapi? k.m. kwenu jikoni
  • Wewe au nyinyi mlikuwa wapi? k.m.shambani mkilima
  • Mlijuaje kuhusu ajali ya moto? k.m. mliuona/mliitwa/mlisikia kamsa, n.k. - Yapi yalitokea?

 

Mfano:

Moto wafilisisha

Mtiririko wa mawazo

- Tulikuwa mtoni tukiogelea

- Kusikia mayowe ya “Moto! Moto!”

- Kuacha kuogelea

- Kutimua mbio kuelekea kulikopigwa kamsa

- Kupata nyumba ya jirani ikiteketea

- Kupata waja wakijaribu kuuzima moto

- Kujiunga nao kujaribu kuuzima moto

- Ndimi za moto kuzidi kuimeza nyumba

- Mwenye nyumba kuzirai kutokana na mshtuko

- Moto kuzidi

- Kufika kwa wazima moto

- Kufanikiwa mwanzo mwanzo kuuwahi moto

- Kuishiwa na maji/moto kusambaa

- Hasira za wanakijiji/kuzomewa na wanakijiji/kuondoka kwa wazima moto

- Kuteketea kabisa kwa nyumba/mali chungu nzima kuangamizwa