Insha kuhusu wizi/uvamizi

Mambo ya kuzingatia:

 • Uvamizi ulitokea wakati upi?
 • Ulitokea wapi? k.m. shuleni, nyumbani, hotelini, safarini, benkini, nk.
 • Hali ya uvamizi k.m. silaha zilitumiwa/damu ilimwagwa/watu waliuawa/ nk.

 

Mfano:

 • Uvamizi nyumbani: Mtiririko wa mawazo
 • Ni wakati wa usiku mchanga.
 • Mnapiga soga huku mkiota moto na watu wa aila yako.
 • Mvua inaendelea kunyesha.
 • Ghafla mlango wa jikoni unagongwa kwa nguvu na kuvunjika.
 • Watu walio na silaha kali kali wajitoma jikoni.
 • Amri zinatolewa na wavamizi.
 • Risasi kufyatuliwa.
 •  Kamsa kupigwa na baadhi yenu.
 • Kujeruhiwa kwa mzazi wako.
 • Wasamaria wema kufika.
 • Ving’ora zaidi kupigwa.
 • Askari kufika.
 • Mapambano kati ya askari na wavamizi.
 • Kutoroka kwa baadhi ya wavamizi.
 • Kukamatwa kwa wengi wao.
 • Kupelekwa korokoroni.
 • Waliojeruhiwa kupelekwa hospitalini.
 • Tamati.