Insha ya tamati

 

  • Katika insha za sampuli hii, mtahiniwa huwa amepewa sentensi ya mwisho/ya kutamatisha.
  • Ni sharti mtahiniwa aisome sentensi ile na kuielewa vilivyo kisha atunge kisa kitakachowiana na sentensi ile ya kumalizia.
  • Katika swali la aina hii, mtahiniwa anatakikana aandike kuhusu yale yaliyotokea hapo awali (mbeleni) hadi afikie kiwango cha kuitumia sentensi ile ya mwisho.

 

Mfano:

Andika insha anayokamilika hivi: … Laiti ningalijua, nisingaliwafuata vijana hao.

 

Zoezi

Andika insha zinazoishia:

1. … kwa kweli arusi hiyo ilikuwa ya kufana.

2. … Hakimu alimaliza hukumu yake.

3. … nilifurahi kufika nyumbani salama salimini.

4. … Tangu siku hiyo sijamwona tena.

5. … hivyo ndivyo nilivyoepuka hatari ile.

6. … Kipenga cha mwisho kilipolia sote tulipoteza matumaini.

7. … Kwa kweli msamaria mwema huyo alinisaidia sana.

8. … Tulifurahi sana tulipofanikiwa kuuzi•ma moto huo.

9. … Kwa kweli ajali hiyo ilisababisha maafa mengi.

10. … kamwe sitaisahau siku hiyo maishani mwangu.

 

Elewa sentensi hii.

Sentensi hii inaonyesha kuwa mhusika anajuta.

Kwa nini watu hujuta? Kwa kutofanya yale mazuri watakiwayo kufanya au kuyafanya mabaya ambayo hawakutakiwa kuyafanya. Yaonekana mhusika aliandamana na rafiki zake na hatimaye akajuta. Labda alikuwa kiamboni akisoma/alikuwa amekanywa kutoenda popote/alikuwa ameelezwa kufanya kazi fulani/rafiki zake walim-pitia/walimshawishi waende waka-cheze/alijifanya bendera kufuata upepo/alirudi nyumbani akiwa amechelewa/hakuwa ametimiza aliyokuwa ameagizwa na mama yake/aliadhibiwa ndiposa akaapa kutoandamana nao tena. Mtahiniwa anaweza kufuata mikondo tofauti tofauti mradi aonyeshe sababu ya majuto yake ya mhusika.