Insha ya mada teule

Mfano:

Eleza maafa ya ukimwi nchini mwako.

UKIMWI NI DONDA NDUGU / JANGA KWA JAMII n.k.

 • Utangulizi: Eleza kwa ufupi jinsi ambavyo ukimwi umekuwa janga maishani.
 • Mwili: Eleza madhara ya gonjwa la Ukimwi - Husababisha kifo - Kuvunjika kwa familia - Watoto kuachwa mayatima – wanakosa malezi, wanakosa mahitaji, wanakosa elimu, wanakosa mapenzi, wanatengwa na jamii, wanateswa, wanakosa mustakabali. 
 • Umaskini – wawele hushindwa kujipatia riziki - Wanapoteza kazi zao - Wanashindwa kukimu mahitaji yao na ya wale wanaowategemea.
 • Gharama huongezeka kwa jamii – dawa, lishe mazishi.
 • Uchumi huzorota - Wafanyikazi wengi hawafiki kazini wanapolemewa na ugonjwa huu. 
 • Upoteaji wa vipawa na taaluma - Watu wenye vipawa huaga dunia - Vijana na wazee walioelimika hupoteza maisha - Kiwango cha utegemeaji hupanda - Wagonjwa waliojikimu hapo awali hugeuka kuwa kupe. 
 • Tamati: Kuwatahadharisha watu wajiepushe na janga la ukimwi na wawasaidie wale ambao tayari wametumbukia katika bahari hii ya maangamizi (Bahari ya Ukimwi).

Zoezi:

Andika insha kuhusu mojawapo ya vichwa vifuatavyo.

 •  Faida za michezo.
 •  Faida za muziki.
 •  Faida na madhara ya utalii nchini.
 •  Kiini cha ajali barabarani nchini.
 •  Kazi niipendayo.

 

Insha hii huhitaji mwanafunzi kutoa hoja za jambo fulani.

k.m. Faida na madhara ya maji, faida na madhara ya miti, umuhimu wa kuhifadhi mazingira, shule yetu n.k.

Katika insha ya sampuli hii, mwanafunzi anatakiwa kuandika mambo ya kweli wala si yale ya kubuni. Ikiwezekana, anastahili kusisitiza hoja zake kwa kutoa mifano inayojulikana au inayoeleweka kitaifa na kimataifa.