Barua rasmi

- Barua rasmi huandikwa kwa shughuli rasmi au za kiofisi kama vile:

  • Kuomba nafasi ya kazi.
  • Kuomba nafasi ya curriculum.
  • Kuomba msamaha kwa jambo fulani k.m. Mwanafunzi amwombapo mwalimu msamaha kwa kutohudhuria curriculum.
  • Kuomba nafasi kutembelea mahali fulani kama vile mbuga ya wanyama, n.k.

 

Barua rasmi huwa ni tofauti na barua ya kirafiki.

Katika barua rasmi, zipo sehemu nane:

  • Anwani: Anwani ya mwandishi. Anwani hii huandikwa katika sehemu ya juu upande wa kulia wa karatasi. Anwani hii hujumuisha: Makao ya mwandishi k.m shule, kijiji n.k. Sanduku la posta (S.L.P.) Mji na tarehe aandikapo barua husika.
  • Sehemu ya pili: Anwani ya mwandikiwa. Anwani hii hujumulisha, cheo au dhima ya mwandikiwa, sanduku la posta na mji. Huandikwa upande wa kushoto laini moja baada ya tarehe.
  • Sehemu ya tatu: Sehemu hii huonyesha ni nani anayeandikiwa barua. Aghalabu, mwandikiwa hurejelewa tu kama: Kwa Bwana au Kwa Bibi.
  • Sehemu ya nne: Lengo. Sehemu hii huonyesha kwa ufupi lengo la kuandika barua ile k.m. KUHUSU: KUOMBA NAFASI YA KAZI
  • Sehemu ya tano: Utangulizi. Aya hii huwa fupi mno na hutumiwa na mwandishi kujitambua na vilevile kusema matakwa yake kwa ufupi.
  • Sehemu ya sita: Mwili wa barua rasmi: Sehemu hii vilevile huwa fupi na kwa muhtasari. Mwandishi huitumia kuelezea (Iwapo anaomba nafasi ya kazi.): -sifa zake, -umri, -ujuzi wa kazi, -tajriba ya kazi n.k.
  • Sehemu ya saba: Hii huwa ni aya ya mwisho ambapo mwandishi hujaribu “kumguza moyo” msomaji wa barua yake. Aghalabu katika aya hii mwandishi huomba matakwa yake yatiliwe maanani.
  • Sehemu ya nane: Hii ndiyo sehemu ya mwisho ambayo huonyesha jina la mwandishi. Sanasana huwa hivi: Wako mwaminifu, (sahihi) Jina.

Mfano wa barua rasmi

Shule ya Muthithi, S.L.P 49, MARAGUA, 10-03-2006. Meneja, Kampuni ya MLO, S.L.P 17, SABASABA. Kwa Meneja, MINT: MAOMBI YA NAFASI YA KAZI Kwa unyenyekevu mkuu, ninaomba nafasi ya kazi ya ubawabu katika kampuni yako. Mimi ni mwanaume wa umri wa miaka ishirini na minane. Nimehitimu elimu ya upili na kufanya kazi za ubawabu katika kampuni mbalimbali. Katika makampuni hayo yote, nimeonyesha bidii, uajibikaji na nidhamu ya hali ya juu. Ukinipa nafasi hii, nitafanya kazi kwa kujitolea wala sitakuvunja moyo. Pamoja na barua hii, nimeandamanisha ushuhuda wa mengi kunihusu. Nitakushukuru ukinipa nafasi ya kunihoji. Wako mwaminifu, Sahihi Soja Mkali ja Chui.

 

Zoezi

  • Andika barua rasmi kwa Mwalimu Mkuu ukimwomba nafasi ya kujiunga na kida to cha kwanza katika shule yake.
  • Andika barua kwa mwalimu ukimwomba msamaha kwa kutohudhuria curriculum bila kumjulisha mapema.
  • Andika barua kwa Meneja wa kiwanda cha kutengenezea maziwa ukiomba nafasi ya kuzuru hapo na kujifundisha mengi.
  • Mwandikie Mwalimu Mkuu wa shule yako ya msingi ukimwomba akuandikie barua ya kukuwezesha kutafuta kibarua cha kufanya.
  • Mwandikie chifu wa kata yako barua ukimweleza matatizo ya uhalifu pale kijijini penu.