Mifano ya vidokezo

 

Mfano:

 • Ajali ya barabarani.
 • Mambo ya kujiuliza.
 • Ulikuwa wakati upi na wewe ulikuwa wapi?.
 • Ajali ilitokea wapi na lini?

Mtiririko wa mawazo:

 • ulikuwa kando ya barabara ukisubiri gari kuelekea shuleni asubuhi hiyo.
 • kuonekana kwa gari likija kwa kasi.
 • kung’oka kwa gurudumu.
 • kushikwa kwa breki.
 • juhudi za dereva kutofua dafu.
 • kuyumbayumba kwa gari.
 • kuanguka kwa gari na kubingirika.
 • kishindo kikubwa kusikika.
 • watu kupiga kite.
 • wasamaria wema kufika.

Mifano ya vidokezo vya insha mbalimbali

Insha kuhusu ajali

Baadhi ya ambayo maswali mwanafunzi anastahili kujiuliza:

 • Ni ajali ya aina gani? k.m. Ajali ya gari barabarani, gari la moshi n.k.
 • Ajali ilitokea wapi? -Ni nini chanzo cha ajabu hiyo?
 • Ajali ilitokea lini?
 • Wakati wa ajali, ulikuwa wapi?
 • Je, ulishuhudia ajali au ulihusika?
 • Ajali yenyewe ilikuwaje?
 • Ni yapi yaliyotendeka pindi tu baada ya ajali?

 

Mtiririko wa mawazo:

 • watu kuumia
 • watu kutolewa garini
 • wengine kufariki
 • kufanyiwa huduma ya kwanza
 • kukimbizwa hospitalini
 • matabibu kufika kwa ambulensi
 • kuendelea kuwahudumia majeruhi.
 • wahasiriwa wachache kunusurika.
 • hali kwa jumla: damu kutapakaa kila mahali, kilio cha uchungu: kilio cha majonzi majeruhi kuwa na nyoyo za kuku
 • kufika kwa polisi
 • kufanya udadisi wao
 • maiti kupelekwa makafani (ufuoni)
 • watu kutawanyika. Kumbuka unaweza kutaja jambo ambalo halikutarajiwa katika mazingira yale ili insha yako ivutie zaidi. k.m. Baadhi ya watoaji huduma za kwanza kugunduliwa wakiwaibia majeruhi na hata waliokufa.