Insha kuhusu ndoto

- Insha ya ndoto humtaka mtahiniwa kuandika kuhusu ndoto, ya kupendeza au ya kutisha/kuogofya au jinamizi.

- Kwa hivyo kabla mwandishi hajaanza kuandika insha yake kuhusu ndoto, ni lazima aelewe swali linamhitaji kuandika kuhusu ndoto ya aina gani?

 

Katika uandishi wa insha ya ndoto yafuatayo huzingatiwa:

 • Kichwa. Insha yako lazima iwe na kichwa.
 • Utangulizi: Onyesha jinsi ulivyoenda kulala au kuanza kulala. Eleza machache tu.
 • Mwili: Eleza kuhusu ndoto yako kuanzia mwanzo hadi ulipozinduka. Daima, kumbuka hujui wakati hasa ulipoanza kuota. Pia, ndoto haikamiliki. Kwa hivyo, utazinduka usingizini kabla ndoto haijafikia mwishoni.
 • Tamati: Kwa ufupi eleza hisia zako baada ya kuzinduka k.m.ulifurahi, uliogopa, ulipatwa na wasiwasi n.k.

 

 

Kuna njia kadhaa za kuulizia maswali ya ndoto:

 •  Unapopewa mada moja kwa moja k.m Andika insha kuhusu jinamizi.
 • Unapopewa sentensi ya mwanzo k.m. Nilikula chajio changu kisha nikaelekea kitandani. Baada ya kulala kwa muda fulani nilijipata…
 • Unapopewa sentensi ya mwisho k.m … kumbe ilikuwa ni ndoto tu au ...nilifurahi nilipogundua ilikuwa ni ndoto au ... nilikasirika nilipogundua ilikuwa tu ni ndoto.

Zoezi

Andika insha kutokana na maagizo uliyopewa.

 •  Andika insha kuhusu ndoto ya kusisimua.
 •  Andika insha inayoishia … kamsa zangu zilimwamsha mzazi wangu. Alipofika, alinipata nikitokwa na jasho. “Kumbe ilikuwa ni ndoto tu!” Mzazi alishanga.
 • Andika insha ya ndoto inayoishia “… Nilitamani sana niipate ndoto kama hiyo tena.”
 •  Andika insha ya ndoto inayoishia … Nilipumua nilipogundua, yote hayo yalikuwa ni ndoto.
 •  Andika insha ya ndoto inayoanza: Sijui nilikuwa nimelala kwa muda upi nilipojipata katika msitu uliojaa wanyama wa kila aina…