Insha ya picha

- Insha ya picha huandikwa kutokana na picha au michoro iliyotolewa. Katika insha ya aina hii, mtahiniwa huwa amepewa picha/michoro kadhaa.

- Mtahiniwa basi hutakikana kutunga insha yake kutokana na picha/michoro ile. Sharti insha atakayotunga ilingane na mawazo yaliyonuiwa kuwasilishwa kupitia picha/michoro ile.

 

Mambo muhimu ya kuzingatia:

  • Mtahiniwa aiangalie na kuielewa picha / michoro ile.
  • Mtahiniwa atunge kisa kinacholingana na picha / michoro ile.
  • Mawazo yake yatiririke kulingana na picha / michoro ile.
  • Mtahiniwa ateue kichwa mwafaka cha insha yake. 5. Mtahiniwa ateue majina ya mhusika/ wahusika wanaoonyeshwa kwenye michoro.
  • Ni muhimu kuelewa kuwa ni sahihi kuandika mambo ambayo hayaonekani kwenye picha/michoro, mradi mambo hayo yakubalike katika mtiririko wa matukio ya mambo

 

Tahadhari:

- Mtahiniwa asirejee picha/ michoro moja kwa moja aandikapo insha yake k.m. ni makosa kusema, “Katika picha /mchoro wa kwanza, pana mtu anayeendesha gari kwa kasi...” Insha ya picha hadithi ni kama insha hizi nyingine. Tofauti ni kuwa, mtahiniwa huongozwa na picha / michoro kuiandika insha yake.

 

Zoezi

Andika insha ukizingatia mfululizo wa picha hizi (A-E)