KCPE 2008 INSHA

Mtungo wa Kwanza

Mtunzi wa insha hii alitumia methali na semi ambazo haziambatani kamwe na mada ya insha. Hata hivyo, ametumia maneno ya Kiswahili.

Alama iliyotuzwa   =   08

Mtungo wa Pili

Mwandishi wa insha hii anaielewa mada ya insha na amejaribu kuishughulia. Amefanya makosa mengi sana ya kisarufi na tahajia. Hakuakifisha kazi yake hata kidigo, na ana athari kubwa ya lugha ya mama.

Alama iliyotuzwa  =   19

Mtungo wa Tatu

Insha hii imeandikwa vizuri. Mwandishi amepanga kazi yake vizuri katika aya. Hata hivyo, amefanya makosa ya kisarufi na hijai kama:

  • Masika tuliokuwa tumeiombea - masika tuliyokuwa tumeyaombea
  • Kiangazi iliyowana - kiangazi kilichowana
  • sote tulikwenda - sote tulikwenda
  • watu wemo ndani - watu waliokuweko ndani

Alama alizotuzwa  -  38

Mtungo wa Nne

Insha hii imeandikwa kwa ustadi mkubwa. Kazi imepangwa vizuri kwa sentensi na aya pamoja na hati inayovutia. Makosa ya aina yoyote ni machache sana. Mtahiniwa amejaribu kueleza yaliyotokea akizingatia mada aliyopewa. Hoja zake zimekamilika. na insha yake amcikoleza utamu kwa matumizi ya semi na tamathali. Kosa la tahajia limeonakana:

Mwitu  -  mwetu

Alama alizotuzwa  -  38