Ukanushaji

Ukanushaji

Ukanushaji ni sawa na kukataa.

  • Ukanushaji wa nyakati Ukanushaji wa kiarifu sawa hutofautiana kutokana na nyakati. Iangalie mifano ifuatayo.

Mtoto anacheka – Mtoto hacheki.

Mtoto amecheka – Mtoto hajacheka. Mtoto atacheka – Mtoto hatacheka. Mtoto alicheka– Mtoto hakucheka. Mtoto hucheka – Mtoto huwa hacheki.

  • Ukanushaji wa kiunganishi “na“ Kiunganishi na hukanushwa kwa kiunganishi wala k.m. Alifika na akapumzika - Hakufika wala hakupumzika.
  • Ukanushaji wa “ku-” ya kitenzi Vitenzi vilivyo na viambishi k u – hukanushwa kwa kuto -k.m. kusoma – kutosoma, kulia – kutolia, kula – kutokula.

  • Ukanushaji wa “ki-” cha masharti Ki– cha masharti pia huitwa ki– cha lazima. Hii ni kwa sababu matokeo fulani lazima yetegemee tukio fulani k.m. Ukisoma kwa bidii utafua dafu (yaani lazima/sharti usome kwa bidii ili ufue dafu).

Ukanushaji  wake ni –sipo-  k.m  M kiniita

nitaitika - M sipo niita sitaitika;  Aki ja ataniona

– A sipokuja  hataniona.

Ukanushaji wa – nge– ya utegemeano

Hukanushwa kwa kutumia – singe – k .m .Ningekuwa na uwezo  ni ngeenda ughaibuni

Nisingekuwa na uwezo nisingeenda ughaibuni.

 

Ukanushaji  wa – ngali–  ya u tegemeano

Hukanushwa kwa kutumia - singali - k.m

Tungalimakinika tungalifua dafu

Tusingali makinika  tu singali fua  dafu.

 

Ukanushaji wa “ndi-” ya kusisitiza

Hukanushwa  kwa  kutumia  -si- ya kukataa

k.m. Kitumbua hiki ndichonilichopika

Kitumbua hiki  sicho nilichopika.

Ukanushaji wa kiarifu chenye  ʻ o rejeshi  mwishoni

Kiarifu hicho hakikanushwi bali kiari

kinachokifuata ndicho  kinachokanushwa k.m

Mtoto achezaye  ninamjua–  Mtoto achezaye simjui.

Ukanushaji  wa k iunganishi  n i huwa  s i

k.m Mkoba huu  ni wangu

Mkoba huu  si  wangu

  • Ukanushaji wake ni –sipo-k.m Mkiniita nitaitika - Msiponiita sitaitika; Akija ataniona –Asipokuja hataniona.
  • Ukanushaji wa –nge– ya utegemeano Hukanushwa kwa kutumia – singe – k.m. Ningekuwa na uwezo ningeenda ughaibuni -Nisinge kuwa na uwezo nisingeenda ughaibuni.
  • Ukanushaji wa –ngali– ya utegemeano Hukanushwa kwa kutumia - singali -k.m. Tungalimakinika tungalifua dafu – Tusingalimakinika tusingalifua dafu.
  • Ukanushaji wa “ndi-” ya kusisitiza Hukanushwa kwa kutumia -si-ya kukataa k.m. Kitumbua hiki ndicho nilichopika -Kitumbua hiki sicho nilichopika.
  • Ukanushaji wa kiarifu chenye •o• rejeshi mwishoni Kiarifu hicho hakikanushwi bali kiarifu kinachokifuata ndicho kinachokanushwa k.m Mtoto achezaye ninamjua – Mtoto achezaye simjui.
  • Ukanushaji wa kiunganishi ni huwa si k.m Mkoba huu ni wangu Mkoba huu si wangu