Nukta za dukuduku

Nukta za dukuduku ( … )

Hutumika:

  • Kuonyeshea kuendelea kwa maelezo fulani k.m. Tukikutana sitamzungumzia kwa kuwa … 
  • Kuonyeshea maelezo yaliyo wazi kwa msikilizaji k.m. Niliamua kurejea kwetu mambo yaliponiendea mrama. Kama mjuavyo, ng’ombe akivunjika guu malishoni … 
  • Kuonyeshea kuwa kuna maelezo mengine yaliyotangulia lakini hayajaandikwa k.m. … na ni kweli lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani likija.