Matumizi ya 'bora' 'heriI'

Matumizi ya bora, heri, afadhali

Maneno haya hutumika kuonyeshea ile hali ya kupendelea jambo, kitu, mtu au hali moja kuliko nyingine.

Maneno haya hutumika mzungumzaji anapotaka kuonyesha kuwa jambo / hali / kitu kinafaa zaidi kuliko kile kingine.

 

Ziangazie sentensi zifuatazo

  1. Ni afadhali ufukara wa mali kuliko wa akili
  2. Ni bora kuwa na afya badala ya kuwa na mali nyingi
  3. Ni heri kuishi mashambani kuliko mijini
  4. Ni afadhali kuwa na elimu kuliko kutokuwa nayo
  5. Ni bora kusema ukweli badala ya kudanganya.