Ngeli ya PA - PA

 • Viarifu vya ngeli hii huanza kwa pa- k.m Darasani panapambwa kwa matayarisho.
 • Vivumishi viwakilishi amba- Sakafuni ambapo anafagia panateleza.
 • 'O' rejeshi sakafuni anapofagia panateleza.

 • Ndi ni ya kusisitiza Hamamuni anapooga ndipo hapa.
 • Si- ya kukataa Hamamuni anapo ogea sipo hapa.
 • Na- ya kirejelei Hapa napo pana watoto wengi.
 • Viashiria/vionyeshi hapa, hapo, pale.
 • Viashiria/vionyeshi radidi hapa, hapa, hapo hapo, pale pale.
 • Kivumishi enye Sokoni penye wateja pana kelele.
 • Kivumishi -enyewe Tuliogelea mtoni penyewe.
 • Kivumishi -ote Mezani pote pana vitabu.

 • Kivumishi -o-ote Nitakaa popote nitakapoonyeshwa.

 • Kivumishi -ngi Hotelini pengi pana starehe.

 • Kivumishi -ngine Alienda hotelini pengine palipompendeza Kiulizi -pi? Mjomba alienda shuleni papi?

 

Matumizi ya viambishi vya PA katika sentensi

1. Kiambishingeli (pa)

Nyumbani pale pananipengeza. - Nyumbani pale panatupendeza.

 

2. Kirejeshi -O (-po)

Shuleni palipofyekwa ni pangu. - Shuleni palopofyekwa ni petu.

 

3. Kiunganifu -A (pa)

Kitandani pa mtoto panafaa. - Vitandani pa watoto panafaa.

 

4. Sifa -enye/-enyewe

Chumbani penyewe pana baridi. - Vyumbani penyewe pana baridi.

Ubongoni penye nia pana njia. - Ubongoni penye nia pana njia.

 

5. Sifa (-ote, -o-ote)

Dukani pote pana bidhaa. - Madukani pote pana bidhaa.

Uwanjani popote mtu hununua bidhaa. - Nyanjani popote panafaa.

 

6. Sifa (-embamba)

Tunduni pembamba pana mende mdogo. - Matunduni pembamba pana mende wadogo.

 

 7. Sifa -ngi, -ngine

Ukutani pengine pana rangi. - Kutani pengine rangi.

Ukutani kwingi kuna rangi. - Kutani kwingi kuna rangi.

 

8. Vivumishi -pa

Jikoni pazuri pakubwa pana mlo. - Majikoni pazuru pakubwa pana mlo.

 

9. Kukanusha hapa

Uwanjani hapo hapana unyasi mrefu. - Nyanjani hapo hapana nyasi ndefu.

 

ZOEZI

Tia sentensi zifuatazo katika ngeli ya mahali (PA) kulingana na kiambishi ngeli ulichopewa mabanoni.

1. Mlango ule una bawabu mkali

2. Mlima wote umetanda ukungu. 

3. Mto ule mkubwa una ngwena wakubwa.

4. Katika kisima kile mna maji safi.

5. Dika nilipendalo lina bidhaa marighawa.

6. Msitu wote ule waliuoalilia jana. 

7. Anayelilima shamba hili hajalimaliza.

8. Gari lile jeupe limeibeba mizigo mingi.

9. Kitanda chako kizuri ndicho nitakachokilalia.

10. Maskani yoyote yakufaayo uyakimbilie, usisite.