Ngeli ya U - ZI

Ngeli ya U-ZI

Ngeli hii inajumuisha nomino za vitu visivyo na uhai. Ngeli hii ina makundi matano ya nomino.

i. Nomino ambazo umoja huanza kwa u na wingi tunaondoa u k.m. unywele, ukuta, ufagio, ufunguo, unyasi, utepe, utosi, ukoo, upote, upenu, upondo, upongoo, upanga, upepeo n.k.

ii. Nomino ambazo umoja huanza kwa u wingi zinaanza kwa ny k.m. uta, ufa, uwanja, uso, uwayo, uzi, uwalio, ugwe.

iii. Nomino ambazo umoja huanza kwa w na wingi huanza kwa ny k.m. waraka, wakati, wembe, wimbo, wayo, waya, wavu, wanja, wanda, wadhifa, waadhi.

iv. Nomino ambazo umoja huanza kwa u na wingi huanza kwa nd k.m ulimi, uele.

v. Nomino ambazo umoja huanza kwa u na wingi huanza kwa mb k.m ubao – mbao, ubavu – mbavu, ubati – mbati, ubale-mbale

 • Vivumishi Kiwakilishi amba- Umoja: Ukuta ambao unakarabatiwa ni mrefu. Wingi: Kuta ambazo zinakarabatiwa ni ndefu.

 • “O” rejeshi Umoja: Ukuta unaokarabatiwa ni mrefu. Wingi: Kuta zinazokarabatiwa ni ndefu.
 • Ndi- ya kusisitiza Umoja: Ufunguo huo ndio wangu. Wingi: Funguo hizo ndizo zetu.
 • Si- ya kukataa Umoja: Ufunguo huo sio wangu. Wingi: Funguo hizo sizo zetu.
 • Na- ya kirejelei Umoja: Utepe huu nao ni imara. Wingi: Tepe hizi nazo ni imara.

 • Viashiria/vionyeshi Umoja: huu huo ule Wingi: hizi hizo zile Viashiria/vionyeshi visisitizi Umoja: uu huu uo huo ule ule Wingi: zizi hizi zizo hizo zile zile
 • Viashiria/vionyeshi radidi Umoja: huu huu huo huo ule ule Wingi: hizi hizi hizo hizo zile zile

 • Kivumishi -enye Umoja: Uzi wenye fundo haushonei vizuri. Wingi: Nyuzi z e n y e mafundo hazishonei vizuri.
 • Kivumishi -enyewe Umoja: Ubao wenyewe unapendeza. Wingi: Mbao zenyewe zinapendeza.
 • Kivumishi -ote Umoja: Waya wote umetumika. Wingi: Nyaya zote zimetumika.

 • Kivumishi -o-ote Umoja: Nitautumia wavu wowote kuvulia. Wingi: Tutazitumia nyavu zozote kuvulia.
 • Kivumishi -ngi Wingi: Jirani amepokea nyaraka nyingi. Kivumishi -ngine Umoja: Ameupokea waadhi mwingine.Wingi: Wamezipokea nyaadhi nyingine

 • Kiulizi -pi? Umoja: Umesoma silabi za ukwapi upi? Wingi: Mmesoma silabi za kwapi zipi? Kiulizi –ngapi? Wingi: Je, ng’ombe ana kwato ngapi?

 • Vivumishi vya idadi Mmoja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi, kumi na mmoja, kumi na mbili, kumi na tatu, kumi na nne, kumi na tano • a1_1 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • a2_2 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • a3 by bartleby.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • a4 by flashbak.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • a6 by mendocinobaby.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • a10 by kesaus.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • a8_1 by mustangsplus.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • a9 by pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.