Vimilikishi

Vimilikishi

Vimilikishi ni maneno yanayoonyesha hali ya kuwa na kitu, yaani kumiliki (ya kutamalaki). Kwa kawaida katika lugha ya Kiswahili, vimilikishi hutegemea hali mbili: nafsi na ngeli ya nomino husika. Ili kuelewa vimilikishi sharti mwanafunzi aelewe kwa kina nafsi zote tatu na pia ngeli zote za Kiswahili. Vimilikishi vya nafsi moja vitabadilika kulingana.

Soma mifano ifuatayo:

  • Mimi nina kitabu kwa hivyo kitabu ni changu. (KI-VI)

  •  Mimi nina rula kwa hivyo rula ni yangu. (I-ZI)

  • Mimi nina daftari kwa hivyo daftari ni langu. (LI-YA)
  •  Mimi nina wembe kwa hivyo wembe ni wangu. (U-ZI)

Nafsi ni ile ile lakini nomino ni katika ngeli mbalimbali ndiposa vimiliki vimebadilika. Vilevile vimiliki vitabadilika kulingana na nafsi ya mmiliki mhusika.

Tazama sentensi zifuatazo:

  •  Mimi nina kitabu. Kwa hivyo kitabu ni changu. (Nafsi ya kwanza)
  •  Wewe una kitabu kwa hivyo kitabu ni chako. (Nafsi ya pili)
  • Yeye ana kitabu kwa hivyo kitabu ni chake. (Nafsi ya tatu) Nomino ni ile ile lakini nafsi ni mbalimbali ndiposa vimiliki vimebadilika.

Muhimu

Katika hali ya umoja:

  • vimiliki vya nafsi ya kwanza vinaishia kwa silabi –ngu, ii. vimiliki vya nafsi ya pili vinaishia kwa silabi –ko
  • vimiliki vya nafsi ya tatu vinaishia kwa silabi –ke Wingi wa vimilikishi Ili pawe na kimilikishi, sharti pawe na angalau nomino mbili au vitenzi yaani nomino miliki na nomino milikiwa.

Basi, iwapo unatakikana kuandika wingi wa vimiliki sharti ukumbuke kuzungumzia nomino zote mbili katika hali ya wingi.

  • k.m Mimi nina kiatu. Kwa hivyo kiatu ni changu
  • . Wingi: Sisi tuna viatu. Kwa hivyo viatu ni vyetu (Wingi wa mimi ni sisi. Nao wingi wa kiatu ni viatu). 

Tazama jedwali  lifuatalo  kwa makini

Nafsi

Ngeli         Nomino                               kwanza         pili            tatu

                                                                (sisi)             (nyinyi)     (wao)

A-W A    watoto                                   wetu           wenu          wao

KI-VI      vyungu                                    vyetu          vyenu          vyao

LI-Y A     mashati                                 yetu             yenu            yao

U-I         mitego                                    yetu            yenu            yao

U-ZI       fito                                           zetu           zenu            zao

I-ZI         nguo                                        zetu           zenu            zao

U-YA     matete                                   yetu            yenu            yao

I-I          damu                                     yetu             yenu            yao

YA-YA   mate                                     yetu             yenu             yao

U-U      ukakamavu                          wetu          wenu             wao

PA-PA  darasani                               petu           penu               pao

KU-KU dukani                                   kwetu        kwenu            kwao

M-M    pambajioni                           mwetu      mwenu           mwao

 

Je,  umegundua  lolote  kuhusiana na silabi  za

mwisho za vimilikishi?

 

Vimilikishimikato

Hivi ni vimilikishi  vinavyokatwa na kisha

k u u n g a n i s h w a   n a   j i n a   l a   j a m a a .   K w akawaida,  ili  tuwe  na vimilikishimikato  au

vimilikishiambata, lazima tuwe na nomino na

kimiliki.

Muhimu

Vimilikishimikato hutumika katika  majina

ya nasaba  pekee.

Kuna njia mbili za kupata vimili-kishimikato:

  •   K u c h u k u a   s i l a b i   y a   m w i s h o   y a

kimilikishi  na kuiunganisha  na nomino

miliki  k.m  mama yangu –  mamangu,

mwana wangu –  mwanangu,  mjomba

wake–  mjombake

  •   K u c h u k u a   i r a b u   y a   k w a n z a   n a   y a

mwisho ya kimilikishi  na kuiunganisha

na nomino miliki k.m  mjomba  wake–

mjombawe,  mama  yako –  mamayo

Tahadhari:

Vimilikishi  vyenye irabu  tatu  havitumiki

katika  vimilikishimikato k.m. mjomba wao,

mama yao