Sentensi

Sentensi ni fungu la maneno linalojitosheleza. Fungu hilo la maneno hutoa maelezo fulani.

Kuna aina mbili za sentensi:

  1. Sentensi fupi k.m. Kalulu anaenda.
  2. Sentensi ndefu k.m. Kalulu anaenda sokoni kununua ndizi, viazi, mahindi na unga kisha apige simu.
  • Sentensi hujumuisha sehemu kadhaa za lugha kama vile nomino, vitenzi, vielezi, visifa n.k
  • Sentensi yoyote ile haiwezi kukamilika bila kuwa na kiarifu. k.m Anasoma.

Kitenzi kinaweza kuongezwa silabi zinazowakilisha mtendaji au mtendewa na pia silabi zinazoonyesha wakati. k.m. Analia, tunacheka, wanalala, niliamka, utasoma, n.k.

  • Vitenzi vikiwa katika muundo huu huitwa viarifu. A (Mtendaji) na (Wakati) soma kitenzi (hali ya kufanya).

Sentensi inaweza pia kuwa na nomino. Nomino ni neno linalotaja jina la mahali, kiumbe, kitu, au hali. Pia huitwa jina au nauni. kiarifu Mwanafunzi anasoma.

  • Nomino kiarifa tunaweza ongeza kisifa katika sentensi. Kisifa ni neno ambalo linafafanua mengi kuhusiana na nomino. k.m Mwanafunzi mtiifu anasoma.

  • Nomino kisifa kiarifa sentensi inaweza ongezwa kielezi. Kielezi ni neno ambalo hutumika kueleza jinsi, wakati, mahali na sababu zinazofanya kitendo kufanyika.
  • Yaani, kielezi huonyesha mengi kuhusiana na kitendo. k.m Mwanafunzi anasoma vizuri.
  • Nomino kiarifa/kitenzi kielezi kiarifu.

  • Vilevile, sentensi inaweza kuwa na kihusishi. Kihusishi sanasana huonyesha uhusiano wa nomino au kitenzi na mahali au nomino nyingine. Yaani, mahali nomino husika ipo au mahali kitenzi husika kinatokea. k.m. Mwanafunzi anasimama kando ya gari. Nomino kitenzi kihusishi nomino.

  • Sentensi inaweza kuwa na kiwakilishi. Kiwakilishi husimamia au hutumika badala ya nomino. k.m. Yeye anasoma kitabu.
  • Kiwakilishi kitenzi nomino.

  • Sentensi vilevile inakuwa na kiingizi. Kiingizi hutumiwa kuonyeshea hisia za mnenaji. Hisia kama vile furaha, huzuni, hasira, na kadhalika k.m. Lo! Kumbe si Kiingizi Kiingizi kiunganishi yeye! kiwakilishi.

  • Sentensi inaweza kujumuisha kiashiria.

Kiashiria (kionyeshei) hutumika kuonyeshea mahali nomino au kitenzi kipo. k.m.

Mwanafunzi huyu anasoma.

[resource: 3162, align: left]

Nomino kiashiria kitenzi.

  • Sentensi inaweza kujumuisha kimilikishi.

Kimilikishi hutumika kuonyeshea “mwenye kitu”. k.m Mwanafunzi huyu anasoma Nomino kiashiria kitenzi kitabu chake. nomino kimilikishi nomino kimilikishi.

  •  Sentensi aidha inaweza kuwa na kiunganishi.

Kiunganishi huunganisha maneno au sentensi. k.m Fatuma na Rehema Nomino kiunganishi nomino wanasoma vitabu vyao. kitenzi nomino kimilikishi.



  • Anasoma by Clipart Panda used under CC_BY-SA
  • f547bd39-8fc3-4222-a9ca-f45618b70f03 by eLimu used under CC_BY-SA
  • image-_3 by ADDITUDE used under CC_BY-SA
  • 5955802a-d9bb-4076-a482-b02654b4f69d by Minority news used under CC_BY-SA
  • d by eLimu used under CC_BY-SA
  • f by mommy brown used under CC_BY-SA
  • gari1 by Mind solo used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.