Ngeli ya I - ZI

Ngeli ya I-ZI

Ngeli hii inajumuisha nomino za vitu visivyo na uhai.

Nomino hizi umoja na wingi wake huwa ni sawa. Isitoshe, nomino hizi ni za vitu ambavyo vinaweza kuhesabika k.m. kalamu, meza, sahani, rafu, linga, saa, rula, nyumba, soksi, karatasi, linga, kamusi, wiki, siku, chaki, chupa, ndizi, kamba, bawaba, pete n.k.

  • Vivumishi Kiwakilishi amba-

Umoja: Nyumba a m b a y o imejengwa ni yako. Wingi: Nyumba ambazo zimejengwa ni zenu.

  • “O” rejeshi

Umoja: Nyumba inayojengwa ni yako. Wingi: Nyumba zinazojengwa ni zenu.

  • Ndi- ya kusisitiza

Umoja: Chupa hii ndiyo iliyobebea maziwa. Wingi: Chupa hizi ndizo zilizobebea maziwa.

Si- ya kukataa Umoja: Chupa hii siyo iliyobebea maziwa. Wingi: Chupa hizi sizo zilizobebea maziwa.

  • Na- ya kirejelei

Umoja: Chaki hii nayo inaandikia vizuri. Wingi: Chaki hizi nazo zinaandikia vizuri.

  • Viashiria/vionyeshi

Umoja: hii hiyo ile Wingi: hizi hizo zile

  • Viashiria/vionyeshi visisitizi

Umoja: ii hii yiyo hiyo ile ile Wingi: zizi hizi zizo hizo zile zile

  • Viashiria/vionyeshi radidi

Umoja: hii hii hiyo hiyo ile ile Wingi: hizi hizi hizo hizo zile zile

  • Kivumishi -enye

Umoja: Nguo yenye kiraka haipendezi. Wingi: Nguo zenye viraka hazipendezi.

  • Kivumishi -enyewe

Umoja: Sindano yenyewe haina kutu. Wingi: Sindano zenyewe hazina kutu.

  • Kivumishi -ote

Umoja: Mtoto amekula chapati yangu yote. Wingi: Watoto wamekula chapati zetu zote.

Kivumishi -o-ote

Umoja: Sitaikubali meza yoyote ile. Wingi: Hatutazikubali meza zozote zile.

Kivumishi -ngi Wingi: Mama aliniletea peremende nyingi.

  • Kivumishi -ngine

Umoja: Nilinunuliwa penseli nyingine ya kuchorea. Wingi : Tulinunuliwa penseli nyingine za kuchorea.

Muhimu

Zingine haiwezi kutumiwa badala ya nyingine (wingi).

Ingine haiwezi kutumiwa badala ya nyingine (umoja) Kiulizi -pi? Umoja: Je, utaifunga tai ipi? Wingi: Je, mtazifunga tai zipi?

 

  • Kiulizi -ngapi?

Wingi: Ni sweta ngapi zilizofuliwa?

 

  • Vivumishi vya idadi

moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi, kumi na moja, kumi na mbili, kumi na tatu, kumi na nne, kumi na tano



  • q11_2 by bbc.co.uk used under CC_BY-SA
  • q7_2 by EDITED & ElIMU used under CC_BY-SA
  • q8_2 by oxfordscholarship.com eLimu used under CC_BY-SA
  • q9_2 by duallayerdvdwallpaper.blogspot.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • q12_1 by tes.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • q13_1 by nation.co.ke & eLimu used under CC_BY-SA
  • q14 by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
  • q50 by smallhomeafrica.blogspot.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • q51_1 by all-free-download.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • q60 by alumni.dixie.edu/benefits/ used under CC_BY-SA
  • q61 by pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.