Vimilikishi mikato

Vimilikishi mikato

Hivi ni vimilikishi vinavyokatwa na kisha kuunganishwa na jina la jamaa. Kwa kawaida, ili tuwe na vimilikishimikato au vimilikishiambata, lazima tuwe na nomino na kimiliki.

Muhimu

Vimilikishimikato hutumika katika majina ya nasaba pekee. Kuna njia mbili za kupata vimili-kishimikato:

  1. Kuchukua silabi ya mwisho ya kimilikishi na kuiunganisha na nomino miliki k.m mama yangu – mamangu, mwana wangu – mwanangu, mjomba wake – mjombake
  2. Kuchukua irabu ya kwanza na ya mwisho ya kimilikishi na kuiunganisha na nomino miliki k.m mjomba wake – mjombawe, mama yako – mamayo

Tahadhari: Vimilikishi vyenye irabu tatu havitumiki katika vimilikishimikato k.m. mjomba wao, mama yao n.k.