Matumizi ya 'na'

Matumizi ya na

“Na” hutumiwa kutolea maana mbalimbali katika sentensi. Kwa mfano

 • -na- ya wakati uliopo Tunasoma kwa bidii Mnaandika vizuri
 • Na ya kiunganishi Juma na Fatuma ni wanafunzi hodari. Kiswahili Teule na Uhondo wa Kiswahili ni vitabu vizuri.
 • -na- ya mnyambuliko – hali yakutendeana, kutendana Wao husaidiana kazini. Sisi tunapendana sana.
 •  Na ya mtendaji Chakula kilipikwa na shangazi.

Majeruhi walisaidiwa na wasamaria wema.

 •  -na ya kumiliki Tuna vifaa vipya. Ana kofia pana.

 • Na- ya ufupishaji na nafsi Nao waliamua kuondoka. Naye alifurahia mwaliko huo.

 •  -Na ya hali Mwalimu ana furaha. Mwanafunzi ana bidii.
 •  Na- ya uhusiano Nguo nazo ni safi. Huko nako ni safi.

Zoezi

Chagua jibu sahihi la kuzikamilisha sentenzi hizi.


1. Kiatu ____ ( nayo, nawe, nacho, nako) huvai kwa nini?

2. Mayai ____ ( nazo,nayo, naye,nao) hutagwa na batamzinga.

3. Jua _____ ( nayo, nalo, nacho, nao)  huwaka sana siku hizi.

4. Likizo ____ ( nalo, nayo, nacho, naye ) tumeanza leo.

5. Maiti ____ ( naye, nayo, nazo, nawo) huzikwa kwa heshima.

6. Viumbe ____ ( nao.nazo, nzvyo, naye) ni mali ya mungu.

7. Chumvi _____  ( navyo, nacho, nazo, nao) hupatikana kila bahari.

8. Tabasamu ____ ( nayo, nalo,nako, nacho) hufurahisha moyo.

9. Vita ____ ( nayo,nazo, navyo, napo) huleta hasara kubwa.

10. Kuoga _____ ( nayo,nalo,nazo, nako) hufaa kila siku. • na_1 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_2 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_3 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_4 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_5 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • na_6 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.